Zinazobamba

TUKIO KUBWA LEO JIJINI HILI HAPA,SOMA HAPA KUJUA







Kaimu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bi SOPHIA MJEMA akimkabidhi cheti mmoja wa maofisa wa jeshi hio waliopewa zawadi kwa azi yao kubwa wanayolifanyia jeshi hilo

Watanzania ambao wanamiliki silaha nchini bila kibali maalum wametakia kuzisalimisha ndani ya jeshi la polisi mara moja kwani umiliki wa silaha hizo ni kinyume na sheria za Tanzania na endapo utakutwa na silaha hio sheria itachukua mkondo wake.
Wito huo umetolewa leo na kaimu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bi SOPHIA MJEMA katika sherehe za utoaji wa zawadi kwa maofisa wakaguzi na askari wa Vyeo mbalimbali wa jeshi la polisi shughuli iliyofanyika katika chuo cha Taaluma ya polisi jijini Dar es salaam ambazo zimetolewa na kamishna wa polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam SULEMAN KOVA.

Akizungumza katika shughuli hiyo kaimu muu wa mkoa wa Dar es salaam Bi SOPHIA MJEMA amesema kuwa hali ya amani katika jiji la Dar es salaam na nchini kwa ujumla itakuwepo endapo wanachi watatii sheria bila shuruti ikiwa ni pamoja na kushirikiana na jeshi la polisi kuwafichua wahalifu hasa wale ambao wanakuwa na silaha za kufanyia uhalifu kinyume na sheria.

Bi SOPHIA amelipogeza jeshi la polisi kwa kuendelea kupambana na uhalifu huo ambapo wamefanikiwa kukamata silaha mbalimbali za kufanyia uhalifu ambapo amewataka kuongeza kasi katika zoezi hilo ili kuhakikisha ulalifu katia jiji la Dar es salaam unakuwa ni jambo la historia tu.
Picha mbili zikionyesha viongozi wa dini mbalimbali ambao walishirika katika mchezo wa moinra wa miguu mwishini mwa mwaka jana mchezo uliochezwa katika uanja wa taifa uliokuwa na lengo la kuahamasisha umoja na upendo miongoni mwa dini hizo waki[okea kombe lao leo mbele ya kamishna kona na kaimu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam

 Aidha akizungumzia swala la baadhi ya wanachi wanaokuwa wanatembea na pesa nyingi kwa pamoja katika mifuko amesema kuwa mtindo huo ni mtindo wa kizamani na  unashawishi uhalifu kwani kwa sasa kuna njia nyingi za kisasa za kusafirisha pesa bila kubebe mabulungutu ya hela ambayo mara nyingi.
Katika zoezi hilo jumla ya maofisa wakaguzi na askari 107 kutoka kinondoni,ilala na temeke wamepewa zawadi na jeshi hilo kwa kazi nzuri wanayolifanyia jeshi hilo.

ENDELEA KUFWATILIA TUKIO NZIMA HAPO CHINI


Wadau wa B-PESA wakiwa katika dhughuli hiyo ambayo nao ni wadau wa kusafirisha pesa kwa njia salama



Maofisa wa polisi ambao leo wamepewa zawadi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya zoezi nzima
Kaimu muu wa mkoa wa Dar es salaam Bi SOPHIA MJEMA akizungumza katika hafla hiyo




Picha za juu zikimwonyesha kaimu mkuu wa moa pamoja na viongozi wengine waliohudhuria katika shughuli hiyo wakitizama baadhi ya silaha zilizokamatwa na jeshi la polisi ambazo zilikuwa zinatumika kufanyia uhalifu mbalimbali katika jiji la Dar es salaam ambapo ni kazi nzuri sana inayofanywa na jeshi la polisi kandda maalum ya Dar es salaam

Hakuna maoni