Zinazobamba

MAWAZIRI WA KIKWETE WAANZA KAZI NA MIKWARA,MRITHI WA TIBAIJUKA ASEMA YAKE,WA MUONGO NAYE PIA SOMA

   Waziri wa Nishati na Madini,Mhe. George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokelewa na uongozi wa Wizara hiyo mapema leo asubuhi. Mhe. Simbachawene amesisitiza umuhimu wa sekta za nishati na madini kama mhimili mkuu wa ukuaji wa uchumi wa nchi na kuomba ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali wa sekta za nishati na madini.

NA KAROLI VINSENT
WAZIRI mpya wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Mandeleo na Makazi,Wiliam Lukuvi ameanza kazi rasmi na kusema hatumuongopa mtumishi yeyote katika wizara hiyo atakayekwenda kinyume na taratibu,basi hatosita kumtimua kazi.
        Kauli ya Waziri lukuvi ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akitamburishwa kwa Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na maendeleo na Makazi baada ya kuteuliwa kwake ambapo alisema anafahamu wizara hiyo imejaa watu wezi,ambao hawako tayari kumsaidia mtanzania.
“Naingia hapa najua kuna watu wanafanya dhuruma kwa watanzania na mabosi wao ni matajiri watu wenye fedha ambao wamegeuza wizara hii kumkandamizia mtanzania na kumnyonya kutokana na matakwa ya matajiri ambao wanawapa fedha”
      “Nataka niwambia kabisa waondoke kabisa mapema kabla sijawafukuza na kuwapelekea mahakamani,maana sitomfumbia macho mtu yeyote na wala sitomuogopa”alisema Waziri Lukuvi.
     Waziri lukuvi aliongeza kuwa tatizo la migogoro ya Ardhi,katika wizara hiyo limekuwa kubwa sana na kusema atapambana nalo na kuhakisha anatatua tatizo hilo.
“Kwanza najua wananchi wa hapa mkoa wa Dar es Salaam,wamesaidiwa sana na Wizara hii,nataka niwambia naingia katika wizara hii,nitakuwa natumia mda mwingi kufanya kazi za mikoani”alisema Waziri Lukuvi.
       Kauli hiyo ya Waziri lukuvi imekuja siku moja kupita baada Rais Jakaya Kikwete kumteua kuwa Waziri kwenye Wizara hiyo,ambapo imetokana na Kujiuzulu kwa Profesa Anne Tibaijuka kutokana na kuingiziwa Bilioni 1.6 na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering Bwana James Rugimalira.
     Kwa upande wake Naibu Waziri mpya wa Wizara hiyo, Angellah Kairuki  akawataka wafanyakazi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuacha uvivu na kusema atawashugulikia watumishi wazembe.

       Naye Katibu mkuu wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo  na makazi Bwana Alphayo J. Kidata   akizungumza kwa niaba ya Wafanyakazi alimkaribisha Waziri lukuvi na kuwasihi wafanyakazi wenzake wampe ushirikiano.
        
MRITHI wa Muongo aliyasema haya
      Waziri wa Nishati na Madini ,George Simbachawene amesema kuwa watanzania wamuamini ataendeleza kwa kasi ile ile katika kuwafikishia wananchi maendeleo kupitia sekta za nishati na madini.

Hayo ameyasema leo wakati alipoanza kazi rasmi katika Wizara hiyo akichukua nafasi ya Profesa Sospeter Muhogo aliyejiuzulu wiki iliyopita,amesema kila mtu sio mkamilifu hata mitume watu wengine hawakumuamini.
        Simbachawene amesema ana uzoefu wa kufanya kazi na kuachana na vyeti kwani vyeti ni ziada lakini kalama ya uongozi ndiyo inayohitajika.

Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini,Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akizungumza nao leo

       Aidha amesema wanaotilia shaka uteuzi wake watakuwa na kigezo lakini kila mtu hawezi kuamini kila binadamu ana mapungufu kwa namna anavyoona mtu.
     Simbachawene amesema atafuatilia usiri wa mikataba lakini sasa anasoma mazingira kwanza na kuweza kuweka bayana suala hilo.
     “Niko hapa watu waniamini kutokana na kazi zangu na watanzania waniamini niweze kufanya kazi niliyoaminiwa kwa niaba ya watanzania wenzangu”amesema Simbachawene.


  

Hakuna maoni