HABARI KUBWA LEO-.CUF WATANGAZA MAANDAMANO MAKUBWA,WAMVAA IGP MANGU,SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni ,Mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana wa Chama cha Wananchi CUF-JUVICUF,Hamidu Bobali, Akizungumza na Waandishi wa Habari leo,jijini Dar es Salaam |
NAKAROLI VINSENT
JUMUIYA ya
Vijana ya chama cha Wananchi CUF-JUVICUF wametangaza kuanzisha maandamano makubwa ya kulaani
vitendo wanavyodai ni vya ukiukwaji wa
Haki za Binadamu kilichofanywa na
Serikali ya Chama cha Mapinduzi CCM,cha kumpiga
Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa Ibrahimu Lipumba na wanachama wao, walipokuwa
kwenye maandamo.
Kauli hiyo JUVICUF imekuja siku moja kupita wakati Bunge likiwa limefunga Mjadala ulioibuliwa na Mbunge wa Kuteuliwa James Mbatia juu ya
kupigwa mwenyekiti wa chama cha Wananchi CUF,Profesa Ibrahimu Lipumba,na Bunge
kufikia maamuzi ya pamoja kuiachia mahakama kutoa hukumu.
Akitangaza Maandamano hayo leo Jijini
Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana wa Chama cha Wananchi
CUF-JUVICUF,Hamidu Bobali,wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo
alisema chama hicho kimepokea kwa masikitiko makubwa uongo ulitangazwa na
Waziri wa Mambo ya Ndani nchi Mathias Chikawe wakati alipokuwa akitoa taarifa
Bungeni.
“Tunasikitika sana juu ya kauli
iliyotolewa na waziri Chikawe ndani ya Bunge jana kwa kuweka uwongo mwingi
kwenye taarifa yake kwa kumsingia profesa wetu kwamba alikiuka sheria, sio
kweli kwani profesa alikuwa sahihi,na
ndio maana tunaandaa maandamano sisi Vijana wa Chama hichi ili kulaani vitendo
vya kinyama na vya kuwapiga viongozi wetu na wanachama chetu”alisema Bobali.
Bobali
alibainisha kuwa Jumuiya ya hiyo vijana kufuatia matukio hayo wanamtaka Rais
Jakaya kikwete kuomba Radhi watanzania juu ya matukio hayo ya kupigwa na
kudhalilishwa pamoja kuuliwa kwa viongozi wetu na jeshi la polisi.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza kwa Makini |
Aidha,Jumuiya hiyo ilimtaka Waziri
wa mambo ya Ndani,Mathias Chikawe,pamoja Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest
Mangu kujiuzulu kwenye Nafasi zao kutokana kitendo chao cha kudanganya Umma kwa
kusema Maandamano hayo yalikuwa hayana kibali.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni