HABARI KUBWA-KUPIGWA KWA LIPUMBA,CUF NA BUNGE WAGAWANYIKA,WABUNGE WA CCM WAWAPONGEZA POLISI SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Profesa Ibrahimu lipumba kiwa kwenye ulinzi wa polisi picha na maktaba. |
NA KAROLI
VINSENT
SIKU moja
kupita baada Mwenyekiti wa Chama cha
Wananchi CUF,Profesa Ibrahimu Lipumba
kupandisha mahakamani kwa kile kinachodaiwa kushawishi wanachama wa
hicho kuandamana na kupelekea jeshi hilo kutimia nguvu katika maeneo ya Mtongani
wilaya ya temeke Jijiji Dar es Salaam.
Nacho Chama cha Wananchi
CUF,kimeibuka na kulivaa jeshi la polisi nchini kasema jeshi hilo linatumiwa na
chama cha mapinduzi CCM,ili kudhoofisha upinzani nchi.
Kauli hiyo imetolewa Leo Jijini Dar
es Salaam na Kaimu mwenyekiti wa Chama cha wananchi Cuf ,Juma Duni Haji,Wakati
wa Mkutano na waandishi wa Habari ili
kuzungumzia kitendo alichofanyiwa mwenyekiti wa chama hicho cha kupigwa na
polisi,ambapo Bwana haji alisema Chama hicho kinalaani vikali kile alichodai ni
hujuma wanachofanyiwa na polisi Kuzoofisha upinzani nchini.
“Cuf-tunalaani kitendo hicho cha jeshi
la polisi nchini kutumika kisiasa kuzuia shuguli halali za vyama vya upinzani
nchini na kuwaruhusu ccm kufanya wanavyotaka bila kubughudhiwa na vyombo vya
dola wala kisingizia vya sababu za kintelijinsia”
“Kumkamata mwenyekiti wetu wa
taifa,kumdhalilisha pasipo kuwepo kwa
maandamano ambayo CUF na viongozi wake walishakubaliana kutofanya”alisema
Bwana Haji.
Bwana Haji aliongeza kuwa licha ya
kulaani kupigwa kwa mwenyekiti wao pia wanalaani kupigwa hata kupigwa
wananchama wao ambao wanadai walikuwa hawana kosa lolote.
Aida,Bwana Haji alibainisha kuwa hata
hoja wanayoisema jeshi la Polisi kwamba chama hicho kilidharau magizo ya jeshi
la Polisi,kuendelea na maandamano hayo kwa kusema sio kweli kwani chama hicho
kilifuata maagizo yote.
Vilevile,Bwana Haji alilitaka jeshi la
polisi kuacha kutumika na chama cha
mapinduzi CCM kwani wanachokifanya hakikubaliki na chama hicho kitachoka
na kuongeza kuwa kuchoka huko kutapelekea Taifa kutotawalika na amani ya nchi
itakuwa imevurugika
Bungeni Mjadala uliendelea Hivi.
Baada ya
Jana Spika Anna Makinda kuliharisha Bunge mara mbili jana ili kupisha Serikali
kupeleka Taarifa kamili ya Jeshi la Polisi kutumia nguvu ya kubwa ya Mabomu
kuwapiga wananchama wa CUF,waliokuwa
wakiandamana kuadhimisha kumbukumbu ya Mauaji yanayodaiwa kufanya jshi la
Polisi huko Zanzibar Januari 26 na 27 Mwaka 2001 na kupelekea vifo vya watu
zaidi ya 30.Bunge hilo lilendelea Leo-
Kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Bwana
Mathiasi Chikawe akitoa Taarifa kwaniaba ya Serikali ambapo alisema Jeshi la
Polisi lilikuwa Sahihi kutumia nguvu kuwatawanya wananchama chama cha Wananchi
CUF kwa madai Jeshi hilo lilitoa taarifa za kubaini kumekuwa kunawatu wanataka
kuvuruga amani kwenye maandamno hayo na chama hicho kikakaida taarifa hizo.
Baada kutoa Tamko hilo kwa niaba ya
Serikali na pia Waziri mwenye Dhamana Jeshi la Polisi nchini.
Ndipo Mwanasheria Mpya wa Serikali Gorge Masanju akamtaka Spika Anne Makinda kuacha kulizungumzia
Suala hilo kwa madai tayari lipo katika Mahakama na kuendelea kufanya hivyo
kugonganisha Mihimili miwili kati ya Bunge na Mahakama.
Kauli hiyo ya AG Masanju ikapingwa na
Spika makinda na Kutaka Majadala uendelee.
Wabunge wakaachangia
Wabunge
walipota kuchangia wa kwanza alikuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu
ambapo yeye alikituhumu chama cha mapinduzi CCM,kwa kulifanya jeshi la polisi
kuwa watu wao na kumuomba Waziri wa Mambo ya Ndani Chikawe ajiuzulu.
“Jeshi letu
letu la polisi limetekwa nyala na element la kifashisti,tena zinaungwa ndani ya
CCM na serikali yake,kumbe tunapigwa kutokana na hao ambao wanasema tupigwe
tu,leo nashangaa waziri chikawe na waziri mkuu kwanini wasijiulu”
“Sheria za
vyama vya siasa zinasema wazi nashangaa huyo waziri chikawe anayesema ambayo
atakiwi kuwepo hapo,sheria haziwapi mamlaka kuvuzuia maandamano’alisema Lissu.
Gwiji huyo wa Masuala ya Sheria nchini
ambaye pia ni Mwanasheria mkuu wa Chadema aliendelea kuongea kwa uchungu
akisema hakuna mbunge wa upinzania asiyepigwa na jeshi la polisi.
“Watu wetu wameuliwa na jeshi la
polisi na mwangosi kauawa na jeshi la polisi leo RPC Kamuanda aliyemua
kupandishwa cheo,watu wetu wameuwa na jeshi la polisi,leo nashangaa waziri huyu
anakuja kudanganya bunge hivi”
“Katika hali
hii lazima bunge lifikie maamuzi la kuwajibishe hao wenye mamlaka wanao hamulu
sisi kupigwa ,ambaye ni waziri mkuu,na mwengine ni Waziri Chikawe nae pia
aondoke kama tulivowaajibisha majizi ya Escrow”alisema lissu.
Kwa upande Mwenyekiti wa kambi ya
Upinzani Bungeni Freeman Mbowe alisema Vitendo walivyofanya Jeshi la Polisi
havikubariki na vinafaa kupigwa Vita.
Wabunge wa CCM wanena.
Kwa upande
wao wabunge wa Chama cha Mapinduzi CCM,walitetea jeshi la Polisi na kusema kama
mtu atakayekiuka sheria apigwe tu.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde alisema jeshi
la Polisi liko sahihi kwa kitendo walichokifanya kwani viongozi wa
CUF,walilenga kuvuruga Amani ya nchi.
Hali ya hewa yachafuka Bungeni
Naye MBUNGE wa Donge, Sadifa Juma
Khamis (CCM) alichafua hali ya hewa Bungeni hapo baada ya kusema Mwenyekiti wa
Chama cha Wananchi CUF,Profesa Ibrahimu
Lipumba ambaye amesema amepigwa na kusema hajapigwa bali amegushwa.
“Huyo anayesema amepigwa
lipumba,hivi kapigwa Yule kagushwa,eti anasema waziri ajiuzulu mtu kagushwa
angepigwa angetembea Yule,eti anajifananisha rais kikwete na Lipumba na Rais
wanafanana sio kweli kwani CUF ni chama ni Saccos ili ile ni Saccos’alisema
Mbunge Khamis Sadifa.
Spika Makinda aokoa Jahazi na kumtaka Mbunge
Sadifa afute kuli yake maana fujo zilianza kutoakea bungeni Ndipo mbunge akatoa
maneno ya Saccos.
Mjadala ulipokwisha.
Kwa upande wake Mtoa hoja
Mbunge wa Kuteuliwa James Mbatia alikubaliana na Bunge kuacha mahakama iachiwe na kusema serikali
inatakiwa iondoe ukiritimba ulioko ndani ya jeshi la polisi kwa kuondoa mfumo
uliopo ambao unaleta mtafaruku kati ya polisi na vyama vya siasa.
Makinda anena.
Spika makinda alimaliza
mjadala huo kwa kusema kanuni ya 47,inahaja kuangaliwa kwamba jambo hilo sio la
dharula bali ni la muhimu na kusema mjadala huo uishia hapo na kuiacha mahakama
kufanya kazi yake.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni