KIPIGO CHA MTANI JEMBE-MANJI ACHACHAMAA NA UONGOZI-AWEKA VIONGOZI WAPYA BOFYA HAPO
PICHANI NI Mkuu wa Idara ya habari na Mawasialiano bwana Jerry Cornel Muro akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar Es Salaam |
Exaud Mtei na Karoli Vinsent
MWENYEKITI wa klabu ya Yanga Yusuph Manji
ameitangaza Sekretarieti mpya ya Uongozi katika Klabu hiyo yenye Maskani Mtaa
wa Jangwani Jijini Dar Es Salaam.
Sektretarieti hiyo ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu Dk Jonas B Tiboroha ambae atafanya
kazi na Mkuu wa Idara ya habari na Mawasialiano bwana Jerry Cornel Muro,Bwana
Omar Kaya yeye anakuwa Mkuu wa Idara ya masoko
Wengineo ni Bwana Frank Chacha anakuwa Mkuu wa Idara
ya Sheria pamoja na bwana Charles Boniface ambae atakuwa Kocha Msaidizi
Akithibitisha Kuteuliwa kwa Viongozi hao wajuu
Klabuni hapo mda huu Jijini Dar Es
Salaam wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari na Mkuu wa Idara ya habari na Mawasialiano bwana
jerry Cornel Muro pamoja na kutangaza Viongozi hao wapya alisema Wanachama,Mashabiki,Wapen
pamoja na wapenzi wa Klabu hiyo
washirikiane na Viongozi hao wapya kuiletea maendeleo Klabu hiyo kubwa nchini.
Aidha,jery Murro alisema Mwenyekiti wa yanga anamshukuru
sana Bwana aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo mbrazili MARCIO MAXIMO pamoja na
msaidizi wake kwa ushirikiano wo waliouonyesha katika timu hiyo na kuwatakia
heri katika maisha yao huko waendako.
Katika hatua nyingine amesema kuwa yanga imeamua
kuongeza vijana katika uongozi wake ili
muda wa kustaafu ukifika yanga iyakuwa na waridhi bora watakaoendeleza mazuri
waliyoyakuta..
Hakuna maoni
Chapisha Maoni