UOZO NA UCHAFU WA SOKO LA MAHAKAMA YA NDIZI HUU HAPA,wakulima wa ndizi hoi....UWAMANDIMA WAKENUA
-->
![]() |
Roli la ndizi ambalo limesheni likisubiri zamu yake kushusha katika soko la nadizi mabibo, soko hilo linaelezwa ndilo soko peke lenye mahakama yake, kwa habari kamili soma hapa |
![]() |
Zamani si rahisi kukuta soko hili likiwa na bidhaa tofauti zaidi ya machungwa sasa ni kawaida baada ya genge la watu wachache kuona kuna mwanya wa kupiga pesa kirahisi |
![]() |
UWAMANDIMA:
CHAMA KINACHOTENGENEZA MABILIONI YA SHILINGI YANAYOINGIA MIFUKONI MWA
WATU WACHACHE HUKU WAKULIMA WAKIZIDI KULIA NA KUSAGA MENO
Katika soko la mahakama ya ndizi jijini Dareslaam,ndilo soko pekee ambalo lilionekana kama mkombozi kwawakulima lakini ukweli ambao fullhabari umefunuriwa ni kwamba chama cha wafanyabiashara wa sokoni hapo limekuwa ni genge la kufadhili wezi, wa ndizi pamoja na ubadhirifu wa mamilioni ya shilingi
Sokoni hapo inaelezwa kunanuka Wizi,
uonevu, ubadhirifu, ubabe na utembo ambalo kwa silimia kubwa umekuwa ukilindwa na chama cha wafanyabishara wa soko hilo wachache wanaojiita UWAMANDIMA
Sikumoja
fullhabari kama kawaida yake ikiwa kazini ilipata simu ya dharula
kutoka moja ya wafanyakazi wa sokoni hapo wakimtaka mwandishi wetu
ende haraka sokoni hapo kuchukua habari,hakika mambo ambayo
yameshuhudiwa nadiriki kusema soko hili huenda liko katka nchi ya
angani ambayo rais wake hafamiki, hakuna mtu anayejali dhurma
inayofanywa na watu wachache waliojingea utamaduni wa utembo ambao
wapo kwa ajiri ya kumnyonyonya mkulima,
Kifupi
soko la mahakama ya ndizi na madudu yake ni haya hapa
Soko
la mahakama ya ndiz linasehemu tatu ambayo imegawanywa kutokana na
bidhaa ambazo huuzwa ambapo kuna sector ya Nyanya, Mbogamboga na
Ndizi. Na kila sehemu kuna uongozi wake ambazo kwa hakika kuna madudy
ya aina yake ndani yake, Fullhabari leo hii imejikita dhaidi katika
sekta ya ndizi ambayo ndiyo unyanyasaji mkubwa umeonekana kukithiri
huku hakuna mtu wa kukomboa hali hiyo,
Upande
huu wa Ndizi soko linaongozwa na chama kimoja maarufu sna wanakiita
“UWAMANDIMA”chama hicho kinaongozwa na genge la watu 356 ambao
hukutana mara mbili kwa mwaka na kugawana posho kubwakubwa kwa kila
mmoja huku mkulima akibaki analia bila sabu yoyote,
MADAI
YA WAKULIMA WA NDIZI SOKONI HAPO
Chama
cha uwamandima kinauongozi wa wa aina yake sana, kuna watu wanajiita
makamanda, wengine mabususu. Watu hawa wameonekana kuwa na madaraja
tofauti ambao hunyonya mkulima kwa style ya aina yake,Leo hii
nitakulezea kwa umakini kuhusu Mnyonyaji namba moja anaykusanya zaidi
ya milioni saba kwa wiki bila kufanya kazi
MAKAMANDA
Hawa
watu kwanza wako 60 tu soko zima ambao kazi yao kubwa haieleweki,
watu hawa wamekuwa wakilelewa kwa muda mrefu na kula fedha za
wakulima bure tena bila kuchafuka, inadaiwa kuwa watu hawa ndio
wanaokula 20,000 ya kila gari inayoingia sokoni hapo,
Utafiti
uliofanywa na fullhabari mpaka sasa, unaonyesha kuwa soko hilo la
mahakama ya ndizi limeendelea kuwaheshimu watu hawa wanaokingiwa
migongo na chama nyonyaji cha UWAMANDIMA ambao hawako tayari kuondoa
genge hili la watu 60
Fedha
zinazopotea kwenda kwa makamanda
Kwa
siku jumla ya gari 30 zinaingia sokoni hapo ambapo kila gari ni
lazima itoe jumla ya shilingi 20,000 kuwapa kamanda wa siku hiyo, na
jioni ikifika kamanda anapitisha mchango kwa wafanyabiashara wote wa
soko hilo kwa kigezo kuwa wanataka kuwalindia na kama hutaki kulipa
ujue mzigo wako mali yao na soko hilo hutakiwi
Katika
mchango huo, wafanya biashara wote wanalipa kati ya 400 hadi 2000 ili
kulindiwa mzigo wako ambapo jumla ya pesa zote kwa siku anazokusanya
kamanda wa siku husika ni kama Milioni na ushehe hivi,
Mpashaji
habari anasema Makamanda huwa wanapeana zamu ambapo kila kamanda
anafanya kazi kwa muda wa wiki moja na kumpisha mwenzake ambaye naye
anakaa kwa muda huo hadi wote 60 wamalizike ndipo zamu inarud tena
kwa kamanda wa zamu ya kwanza,
Hesabu
zilizopigwa kwa wiki kamanda anaweka kibindoni jumla ya milioni saba
(7,000,000) ambazo anaiba kutoka kwa mkulima mlala hoi,
Ukamanda
unapatikana vipi
Mtoa
habari anasema, si rahisi kuukwaa UKAMANDA katika soko la MAHAKAMA YA
NDIZI, kuupata ukamanda ni sawa na kuuaga umaskini.
Kwanza
ili uwe kamanda Ni lazima uwe mwanachama wa Uwaamandima, lakini napo
si rahisi kuwa mwanachama wa uwamandima.
Watafiti
wa soko hilo wanasema Ukamanda unarithisishwa kama ulivyo urithi
mwingine wowote ama unaweza kuununua kama kuna mtu mmoja wapo toka
kwenye genge la watu wachache hao kutaka kuuza jina lake,
Utafiti
uliofanywa na fullhabari umebaini kuwa tayari kuna watu kadhaa na
ushahidi tunao, wamesharithishwa ukamanda katika soko hilo na
wanaendelea kupiga pesa tena bila kulipa kodi,
Wakati
tukiendelea kulimulika soko hilo kwa siku za usoni tutawawaletea
makala tosha ya kuelezea jinsi serikali inavyopoteza mabilini ya
shilingi kutoka soko hili kubwa linalonyonya wakulima,
BEI
YA UKAMANDA
Ukamanda
unanunuliwa kwa jumla ya shilingi milioni tano 5,000,000, na kama
hauna huwezi kuupata ukamanda, tena siyo kila mtu anaweza kununua
ukamanda, ni lazima uwe mmoja wa genge la watu wa UWAMANDIMA ndipo
uwe umekizi vigezo vya kupata ukamanda
Mabususu
wao ni watwana wa MAKAMANDA ambao huwatumikisha kazi ngumu huku
makanda wakila kuku kwa mrija
Hakuna maoni
Chapisha Maoni