Vyama vya Siasa viliitisha maandamano yakadhibitiwa na Polisi, Bungeni walilindwa na Polisi wenye farasi na magari ya deraya. Mimi naanza kushawishika kwamba safari ya CCM ndio sasa imeiva maana hata farao alipoona wana wa Israel alitumia mbinu na mabavu kama wafanyavyo CCM leo hii.

Mfalme Sauli alipokwisha nyang'anywa upako wa utawala ilimlazimu kumwinda kijana Daudi usiku na mchana akidhani nguvu zake zitabadili mtazamo wa Mungu. Kama ilivyoandikwa kwenye maandiko Kitabu Kitakatifu kuhusu Mfalme Belishaza alioona Maandiko yameandikwa ukutani akashindwa kuyasoma, akawatafuta waganga, nao wakashindwa kuyasoma ndipo akamwita Daniel.

Anachokieleza Jaji Joseph Sinde Waryoba watu wote wa CCM hawawezi kukielewa hata kama mtatumia maguvu kiasi gani. Watakachoweza kukielewa ni deal za Ufisadi, matumizi ya waganga kama walivyoletwa kwenye Bunge la Katiba, na kule walikokimbilia wakati wa Babu wa Lodiondo kwenye Kikombe.

Mzee Waryoba tunakuombea kwa Mungu uendelee na kazi hii ya manufaa kwa wanyonge. Ikumbukwe kwamba Ninyi watu wa Mkoa wa MARA ndio waasisi wa Ukombozi na Uhuru wa wanyonge. Mwalimu alijitolea maisha yake yote hakuwa mtu mbinafsi. Tunaamini sasa kupitia kwenye taasisi ya Mwalimu Nyerere na ninyi wazee wetu wenye maisha manyoofu ambayo hayana tuhuma zozote kuhusu ufisadi, rushwa na ukandamizaji.

Tunaomba Mfuko wa Mwalimu Nyerere utoe namba za AKAUNTI ili watanzania wenye kuchoshwa na UKOLONI wa CCM wachangie ukombozi ili mwende kila kona ya nchi hii kutoa elimu hii ya Muhimu ili kujikomboa na mkoloni mweusi.

Tunawaomba wanahabari watusaidie kuandika kwa kina mapungufu yaliyomo kwenye Katiba pendekezwa. Ikiwezekana anzeni kutuandikia vipeperushi kutuelezea mapungufu ya ibara kwa ibara. Wanaharakati jitokezeni kumuunga mkono mzzee Joseph Waryoba, Mwalimu Nyerere Foundation kutuelimisha kwa kasi.

Hizo Katiba pendekezwa tutazisikia kwenye radio tu maana hazijagawanywa kwa wananchi. Sasa kama hawajampelekea Mzee Waryoba wewe na mimi tutaipata kweli?