Zinazobamba

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI BARABARA YA BAGAMOYO - PANGANI - TANGA NA DARAJA LA MTO PANGANI (M 525)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo (Makurunge)  - Pangani - Tanga: sehemu ya Mkange - Pangani - Tanga (km 170.8) kwa kiwango cha lami pamoja na Daraja la Mto Pangani (m 525) na barabara unganishi (Km 25) kwa kiwango cha lami Mkoani Tanga, leo Februari 25, 2025.

Ujenzi wa Barabara hiyo ni sehemu ya Barabara za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inayounganisha nchi mbili za Kenya na Tanzania kwa ukanda wa Pwani. 

Aidha, Barabara hiyo ipo kwenye ushoroba wa Pwani ya Afrika Mashariki unaoanzia katika Mji wa Malindi na kupitia Miji ya Mombasa na Lungalungakwa upande wa Kenya na Horohoro, Tanga, Pangani hadi Bagamoyo kwa upande wa Tanzania.





Hakuna maoni