KAMPUNI YA PLANET ONE GROUP YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI TANZANIA*
*Dodoma*
Imeelezwa kwamba Tanzania ni moja ya nchi katika Bara la Afrika iliyobarikiwa na wingi wa aina mbalimbali za rasilimali madini ambazo zimekuwa kivutio kwa kampuni za uwekezaji kutafuta fursa katika mnyororo wa thamani madini.
Hayo yameelezwa leo Februari 26, 2025 na mjiolojia Ambreesh Jha ambaye ni Mjiolojia Mkuu wa Idara ya migodi na utafiti katika kampuni ya Platnet One Group yenye makao makao makuu yake Dubai.
Ambreesh amesema kuwa, Planet One Group imevutiwa na uwepo wa jiolojia nzuri nchini Tanzania inayoonyesha aina mbalimbali za madini kulingani ukanda wa jiolojia ya sehemu husika ikiwemo ukanda wa madini ya metali, kimkakati , vito pamoja na madini ya mbolea.
Akielelezea kuhusu uwekezaji wa kampuni ya PlanetOne-Group Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Biashara Manoj Kumar Singh amesema kuwa, kwa kipindi kirefu kampuni ya Planet One Group imejikita katika utafiti na uwekezaji kwenye rasilimali asili ikiwemo uchimbaji na utafiti wa madini pamoja na uzalishaji wa mafuta na gesi barani Afrika kama vile nchi ya Ghana, Senegal, Cameroon, Siera Leone, Msumbiji na Bostwana.Singh ameongeza kuwa, kutokana na fursa za uwepo wa madini mbalimbali nchini Tanzania kampuni ya Planet One Group imeamua kutafuta fursa ya uwekezaji katika Sekta ya Madini.
Awali, Naibu Katibu Mkuu, Wzara ya Madini Msafiri Mbibo akiwakaribisha wawakilishi kutoka kampuni ya PlanetOne- Group amewaeleza kuwa, Tanzania inaendelea kutafuta wawekezaji kwenye mnyororo wote wa thamani madini kwa kutengeneza mazingira bora yatakayovutia wawekezaji Duniani kote lengo likiwa ni kuifanya Sekta ya Madini kuwa muhimili mkubwa wa kiuchumi katika kuleta maendeleo endelevu nchini.Mbibo amefafanua kuwa, Tanzania ina madini ya aina mbalimbali yakiwemo madini vito, madini ya mkakati na madini ya mbolea ambayo yanatoa fursa mbalimbali kwa wageni kuja kuwekeza, hivyo ameitaka kampuni ya PlanetOne kuja mpango mkakati unaonesha namna wanavyotaka kuwekeza kwenye Sekta ya Madini nchini kwa kushirikiana na Serikali.
*# MadiniNiMaishana Utajiri*
*# MineralValueAdditional*
*#InvestInTanzania*
Hakuna maoni
Chapisha Maoni