DKT. MPANGO ATOA POLE NYUMBANI KWA WAZIRI MOHAMED MCHENGERWA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amefika kutoa pole nyumbani kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa Masaki Jijini Dar es Salaam, kufuatia kifo cha Baba yake mzazi Alhaj Omary Mchengerwa.
Makamu wa Rais ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huo na kuwaombea faraja ya Mwenyezi Mungu katika kipindi kigumu cha msiba huo.
Alhaj Omary Mchengerwa amefariki dunia alfajiri ya tarehe 24 Februari 2024 akiwa kwenye Ibada katika Mji Mtukufu wa Medina na kuzikwa tarehe 24 Februari 2024 saa kumi na mbili jioni baada ya Salatil Magharibi katika Makaburi ya baQii Msikiti wa Mtume Muhammad (SAW) katika Mji Mtukufu wa Medina Saudi Arabia.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni