CCM yakionya ACT kutochochea fujo Zbar
Na Mwandishi Maalum Zanzibar
Chama Cha Mapinduzi (CCM )kimekitaka ACT Wazalendo kuacha kueneza upotoshaji na kudai kuwa Uandikishaji wapiga kura Mikoa wa Kaskazini " A" na 'B' kuna baadhi ya wananchi hawakuandikishwa.
CCM kimekanusha na kusema wananchi wote waliokidhi vigezo kwa vya sheria ya Ukaazi na majina yao yamo kwenye Daftari la Sheha wa shehia, wote ameandikishwa.
Indhari hiyo imetolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Mbeto Khamis Mbeto , akimkanya Naibu Katibu Mkuu ACT Wazalendo Zanzibar, Omar Ali Shehe .
Mbeto alimtaka Shehe aache kutoa madai ya kutengeneza kinyume na ukweli dhidi ya watendaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC ), Kamati za Ulinzi na Usalama Mikoa , Wilaya na Makatibu Tawala SMZ kila wanapotimiza majukumu yao ya kazi .
'Shehe kila wakati amekuwa kiongozi kichefuchefu anayekusudia kuvuruga taaswira ya utulivu katika uandikishaji wapiga kura. SMZ ina Vyombo vyake vya kiserikali kuanzia Shehia hadi Serikali Kuu" Alisema Mbeto
Alisema kwa kiongozi anayejua mgawanyo wa madaraka wa serikali , hawezi kumzuia Mkuu wa Mkoa , Wilaya, Polisi , Maafisa wa Usalama au Makatibu Tawala wilaya na Mikoa,wasitimize wajibu wa kazi zao .
Mbeto alisema Omar Shehe yaonyesha hatambui hadhi ya vyombo hivyo na pengine haujui hata muundo wa Serikali , hivyo amekuwa akilipuka na kutoa shutuma, akieneza uzushi na kufanya upotoshaji wakati zoezi la Uandikishaji likiendelea vizuri.
"Kinachofanywa na Omar Shehe ni utekelezaji wa mpango mkakati wao batili kuelekea Uandikishaji Wilaya na Mikoa mingine ya Unguja . Anatamani uzuke mtafaruku. Wanaochochea na walioandaliwa kufanya fujo watajulikanav" Alieleza
Mbeto katika maelezo yake alisema ACT wanajiandaa kuvunja sheria kwa kujaribu kutaka kuwazuia watanzania waliotimiza vigezo vya kisheria baada ya kukaa Zanzibar miaka kumi mfululizo jambo ambalo si sahihi kwa mujibu wa sheria.
"Sheria Namba 4 ya Mwaka 2018 imetaja mzanzibari aliyeishi kwenye jimbo na shehia miezi thelathini na sita mfululizo ataandikishwa kuwa mpiga kura. Kwa Mtanzania anayetoka Aisha Mara ,Njombe, Sumbawanga au Mbeya aliyeishi zanzibar miaka kumi mfululizo nae haki ya kuansikishwa na kupiga kura " Alieleza Mbeto
Mwenezi huyo CCM, alisema mara kadhaa , amekuwa akimsihi sana Shehe aepuke kutoa matamshi hatarishi badala yake aonyeshe ukomavu wake kisiasa lakini amekuwa akijifanya haambiliki na hamnazo.
"Zoezi la Undikishaji linaendelea vizuri .CCM imeshakusanya ushahidi wa matamshi ya vitisho yaliotamkwa na viongozi wa ACT kwenye mikutano ya hadhara .Tumevijulisha vyombo vya dola vipime matamshi hayo na kuchukua hatua mapema " Alieleza Mbeto
Hakuna maoni
Chapisha Maoni