DC HAPI ACHARUKA ,APIGA 'STOP' BOMOABOMOA,SOMA HAPO KUJUA
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi amepiga marufuku ubomoaji wa nyumba bila idhini yake.
Pia, ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata madalali wa Mahakama wanaotumiwa
kubomoa nyumba za wananchi bila kupata kibali kutoka kwake.
Amesema hayo leo Jumatano, alipozungumza na wananchi wa Kata ya Kunduchi
alipotembelea eneo hilo akiwa ziarani kikazi kusikiliza kero za wananchi na
kukagua miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa Soko la Samaki.
Marufuku hiyo imetolewa baada ya Diwani wa Kunduchi, Michael Urio kutoa kero
kwamba kuna watu wamevunjiwa nyumba pasipo viongozi wa maeneo husika
kushirikishwa.
Hapi amesema kumekuwa na kesi nyingi ofisini kwake kuhusu kubomolewa
nyumba na watu aliowaita matapeli na kwamba, kuanzia sasa hakuna atakayebomoa
bila ya yeye kujua.
Amesema lengo ni kuhakikisha nyumba zinazobomolewa zimeainishwa na
Mahakama kwa kuwa madalali wengine wanaghushi hukumu.
"Ni marufuku mtu kuvunja nyumba bila mimi na vyombo vyangu kuwa na taarifa.
Hatuwezi kuvumilia huu mchezo, kama kuna dalali amekwenda kuvunja nyumba
ambayo haijaainishwa kwenye hukumu ya Mahakama akamatwe mara moja," amesema.
Hapi amesema, "Zipo kesi zimetokea kwenye wilaya yetu, wale madalali wamekuwa
wakivunja nyumba ambazo hazijaainishwa, Mahakama inasema nyumba namba 13
wao wanavunja nyumba namba 23," amesema.
Katika hatua nyingine DC Hapi amechoma nyavu haramu zenye gharama ya shilingi
milioni 20, huku akisitiza uvuvi unao fuata sheria, na kusisitiza kuwa kwa kushirikiana
na ubalozi wa Sri Lanka kupitia balozi wake Lal Silva amehaidi kuisaidia Tanzania
vifaa vya kisasa vya uvuvi na kutoa mafunzo kwa wavuvi.
" Niwaombe wavuvi mjiunge katika vikundi ili muweze kufikiwa vizuri na fursa
za kiuchumi na tuondokane na uvuvi uliopitwa na wakati wa kutumia vifaa duni,
tujiandae mapinduzi ya uvuvi wa kisasa yanakuja, nashukuru serikali ya
Sri Lanka wako tayari kutusaidia nitatuma maombi rasmi na tukikutana
kupitia vikundi vyenu tutaangalia namna ya kuzitumia fursa hizo" Alisema
T
DC HAPI ACHARUKA ,APIGA 'STOP' BOMOABOMOA,SOMA HAPO KUJUA
Reviewed by Unknown
on
19:19:00
Rating: 5