Zinazobamba

BASHITE AZIDI 'SULUBIWA''MEYA WA UKAWA UBUNGO ASEMA LIWALO NA LIWE,SOMA HAPO KUJUA

MEYA wa Manspaa ya Ubungo, Bonface Jacob amesema anakabiliwa vitisho na vishawishi mbalimbali ili kuhakikisha anafuta kesi aliyoifungua dhidi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ya kughushi vyeti, anaandika Faki Sosi.
Makonda anatuhumiwa kudanganya na kutumia vyeti ambavyo siyo vya kwake, na kwamba yeye jina lake alilopewa na wazazi wake ni ‘Bashite’
Hata hivyo, hakuweka bayana anapokea vitisho kutoka kwa nani pamoja.
Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya kutoka kwenye ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma amesema kuwa Mkuu wa Mkoa huyo amekiuka sheria za utumishi wa umma.
“Nimemfungulia shuri la kughushi vyeti pamoja na kula kiapo mbele ya Rais kuwa Mkuu wa mkoa wakati akijua jina siyo la kwake ambalo sio la kwake kinyume cha sheria ya viongozi na watumishi wa umma”, amesema Jacob.
Amesema kuwa tayari kuna viashiria vya ushawishi kutoka kwa watu wa Makonda wanaotaka akubali kuondoa shauri hilo.
Ametaja vitisho anavyokabiliana navyo ni pamoja na kusingiziwa kwamba anatumia ofisi kufanya mikutano ya kisiasa.
Fuatilia Video Chini kujua kilichozungumzwa na Meya Boniface Jacob