Zinazobamba

ALIYEMTOLEA BASTORA NAPE AICHANGANYA SERIKALI YA JPM,MWIGULU NCHEMBA AIBUKA NA "KIHOJA HIKI",SOMA HAPO KUJUA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amesema aliyemtishia bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, hakuwa askari
Waziri nchemba amebainisha hayo leo akizungumza na kituo cha Televisheni cha Clouds, amesema mtu huyo  alikuwa ni mhalifu aliyetumia nafasi ya mkutano wa Nape na waandishi habari kutaka kumpiga risasi lakini aliishia kumtishia bastola.

“Awali tulidhani yule kijana ni polisi lakini hakuwa na sare za polisi, cha kwanza nilimuelekeza Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) kufuatilia na akaleta majibu kuwa hakuwa polisi,” amesema Nchemba.

Aidha, amesema suala la aliyekuwa msaidizi wa Mwenyekiti nwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, Ben Sanane ni ngumu kulisemea kwamba amefariki au yuko kwani polisi bado wanaendelea na uchunguzi.

“Kwa aina ya taarifa ninazopata ni kama inaelekea kufikia ukomo ni jambo ambalo tumelipa uzito kulifanyia kazi na Mtanzania yeyote mwenye nia njema anaweza kutusaidia kufuatilia,” amesema