Zinazobamba

RAIS MAGUFULI AENDELEA KUTENGUA,ATENGUA UTUEZI HUU,SOMA HAPO KUJUA

Rais John Magufuli ameendeleza ‘panga pangua’ ya watumishi wa umma katika nafasi mbalimbali ambapo mchana wa leo ametangaza kummg’oa Diwani Athumani, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), anaandika Charles Willliam.
Rais Magufuli amemuodoa DCI Atumani ambaye aliteuliwa kushika wadhifa huo tarehe 03 Mei, 2015 na Jakaya Kikwete, rais mstaafu wa awamu ya nne ambapo alikuwa akijaza nafasi iliyoachwa wazi na Robert S. Manumba ambaye alistaafu kwa mujibu wa Sheria.

Taarifa ya Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu Kiongozi iliyotolewa mchana wa leo tarehe 29 Oktoba, 2016 haijaeleza sababu za Athuman kuondolewa katika nafasi hiyo.
“Diwani Athuman atapangiwa kazi nyingine na kufuatia uamuzi huo na uteuzi mpya wa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai utatangazwa baadaye.” Imeeleza taarifa hiyo.