JAKAYA
Mrisho Kikwete, Rais mstaafu wa awamu ya nne amesema kuwa asingependa
kuhusishwa na ukosoji wa utendaji wa serikali ya awamu ya tano iliyo chini ya
Rais John Pombe Magufuli, anaandika Charles William.
Kikwete
ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ikiwa ni siku nne
tangu anukuliwe na vyombo mbalimbali vya habari akisema maendeleo hayana maana
ya kuharibu mazuri uliyoyakuta jambo lililohusishwa na kumkosoa Rais
Magufuli.
“Nimestaafu
naomba niachwe nipumzike. Nisingependa kuhusishwa na siasa za mtandaoni dhidi
ya Serikali. Namuunga mkono Rais na serikali yake,” ameandika leo Kikwete.
Katika
kutilia msisitizo Kikwete amesemema, “Nasikitishwa sana na matumizi mabaya ya
picha zangu mtandaoni hususan watu kunilisha maneno kwa kutaka kutimiza malengo
yao ya kisiasa.”
JK
alisema nini UDSM mpaka kuzua mjadala mitandaoni na katika vyombo vya habari
kiujumla?
Rais
mstaafu Kikwete ambaye pia ndiye mkuu wa chuo hicho alikuwa akihutubia ndani ya
ukumbi wa Nkurumah katika maadhimisho ya miaka 55 ya kuanzishwa kwa UDSM
alieleza yafuatayo katika sehemu ya hotuba yake;
“Lazima
ukishakuwa mpya watu waone kama kuna mambo mapya, lakini mapya ya maendeleo
(akasita na kucheka..), siyo mapya ya kubomoa kule tulipotoka.”
Kauli
hii ilitafsiriwa kama ni kuikosoa serikali ya Rais Magufuli kwa namna ambavyo
imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kufumua mfumo wa utendaji uliokuwepo
katika awamu iliyopita hata kama baadhi ya mambo hayo ni mazuri.
Baadhi
ya mambo yanayotajwa kuwa yalikuwa mazuri lakini Serikali ya Rais Magufuli
imeamua kuyabadili ni kurushwa kwa matangazo ya Bunge ya moja kwa moja (live),
kutoa uhuru kwa vyombo vya habari na kuruhusu mikutano ya hadhara, kutofukuza
wafanyakazi bila kuwapa haki ya kujitetea pamoja na kutoa mikopo ya vyuo vikuu
kwa wanafunzi wengi zaidi.
KIKWETE AJITETEA KWA RAIS MAGUFULI,AIRUKA KAULI YAKE ALIYOISEMA UDSM,SOMA HAPO KUJUA
Reviewed by Unknown
on
19:56:00
Rating: 5