CHADEMA YAMUUMBUA OLESENDEKA,SOMA HAPO KUJUA
Baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia msemaji
wake Christopher Ole Sendeka kusema kuwa aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais
katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Edward Lowassa, kuwa si tishio kwa CCM.
Jumamosi ya Oktoba, 29 Chadema imejibu kuwa Lowassa
pamoja na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) utaendelea kuwa tishio kwa chama
hicho na kwamba CCM ijiandae kuachia madaraka mwaka 2020 kwa kuwa imejipanga
kuchukua dola.
Mkuu wa Idara ya Uenezi Chadema Taifa, Hemed Ali
wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho,
jijini Dar es Salaam amesema Lowassa ni tishio kwa kuwa alipokihama chama hicho
aliacha mpasuko na kudai kuwa aliondoka na nguvu ya chama hicho.
“CCM wana homa kubwa iitwayo
Lowassaphobia na ndio maana imeacha kuendelea na shughuli zao na kumuandama
Mjumbe wa kamati kuu wa chama chetu Lowassa. Kimsingi mchakato wa kumpata
Mgombea Urais na Mgombea mwenza wa chama chetu ulikuwa wa kidemokrasia kwa
mujibu wa katiba yetu ambapo ibara (7.7.16 (a) kamati kuu inapewa mamlaka ya
kuwafanyia utafiti wagombea Urais wa chama chetu na kupeleka ripoti Baraza kuu,
“Baraza kuu la chama kwa mujibu wa
katiba ( 7.7. 13 (a)) inapendekeza majina ya wagombea au mgombea aliejitokeza
na hatimae kwa mujibu wa katiba (7.7.10 (c)) Mkutano mkuu wa chama utachagua
mgombea Urais na Mgombea Mwenza,” amesema na kuongeza.
” Lowassa alipitia hatua zote kama
mwanachama halali wa CHADEMA mwenye haki sawa na mwanachama yeyote kwa mujibu
wa katiba (5.1) na (5.2) kimatendo na kiimani kwa kufuata katiba , nilitaraji
Sendeka aeleze kile kiini macho cha kumchagua Ndugu Magufuli Dodoma kuwa
Mgombea wao huku wenyewe kwa wenyewe wakipinga mchakato wa kumpata usiofuata
katiba na kanuni za chama hicho kama walivyojitenga na uamuzi huo baadhi ya
wajumbe wa kamati kuu ile kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa maamuzi
ndani ya vikao.”
Amedai kuwa, Kamati Kuu yao ilipasuka katikati baina
ya wajumbe wake na kudai kuwa wajumbe waliokuwa wanamuunga mkono Lowassa, wengi
wao hawakuchaguliwa kushika nyadhifa serikalini .
“Ni kawaida ya CCM kuchafua mtu ambae
atakua na msimamo na nia ya kulivusha taifa , Wamefanya hivyo kwa viongozi wetu
wa chama na watu binafsi hivyo hatushangai walivyo mshambulia Lowassa akiwa
ndani ya CCM na hata Sasa CHADEMA. Sendeka amesema kuwa yupo kiongozi ndani ya
chama chetu aliyepata dola milioni 15 takribani bilioni 33 eti apangesafu ya
uongozi ndani ya chama,
“Kiuhalisia na kwa hesabu ndogo tu ni
kuwa pesa hiyo si tuu kuwa inatosha kwa ajili ya kupanga uongozi ndani ya chama
bali ni inatosha kwa ushindi wa mitaa, kata na halmashauri , ubunge na urais
hivyo wakati anataja tarakimu hizo ajue na michanganuo ya kimahesabu badala ya
kuwa mkurupukaji na ningemuelewa kama angekuja hadharani kuaga rasmi kwa niaba
ya chama chake na kutupisha kuwatumikia watanzania kuliko kuongea uongo,”
amesema.