WAZIRI MBARAWA ATANGAZA KIAMA WATENDAJI WA TANROAD,ASEMA ATAKUWA MBOGO ZAIDI YA MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA

NA KAROLI VINSENT
WAZIRI wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi,Profesa
Makame Mbarawa amewatangazia kiama watendaji wa Wakala wa barabara nchini,(TANROAD)
kwa kusema hatasita kumchukulia hatua kali kwa mtendaji yeyote atakaye kwenda kinyume na kasi
ya Rais John Magufuli,
Hata hivyo Waziri Mbarawa amewaonya wakandarasi wa
barabara nchini ambao wamezoea kutengeneza barabara zenye chini ya kiwango kwa
kuwaapia atakula nao sahani moja.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na Viongozi pamoja na wakandarani kutoka
ndani ya (TANROAD) alipofanya ziara ya
ofisi hapo,ambapo amesema kwa sasa ndani ya ofisi za wakala wa barabara
kumekuwa na watu wasiokuwa waaminifu ambao wanahusika kutengeneza barabara
zisokuwa na viwango ambazo zimekuwa zikitumika garama kubwa huku baadae kwa mda
mfupi zikiharibika na kuipa serikali hasara kubwa.
“Leo mtandaji anaaminiwa na serikali kwa kusimamia
barabara unakuta mtendaji huyo anashirikiana na watendaji wa serikali ili
kuhujumu barabara nchini,sasa nataka niwaambie kuwa sahivi nitakuwa mkali,na
kama mtu unakaidi basi sitashindwa kukuchukulia hatua kwani utakuwa unarudisha
kasi ya Rais wetu”amesema Waziri Mbarawa.
Waziri mbarawa amewataka wakandarani kushirikiana
katika ujenzi wa kwanza wa barabara ya juu yaani (Frayover)ambayo ni kwa mara
ya kwanza inajengwa nchini hususani mkoa wa Dar es salaam kwa kuwataka
kuonyesha ushirikiano wa juu kwa wakandarasi wakigeni ili kuhakikisha ujenzi
huo unakamilika salama.
Aidha,Waziri Mbarawa aliwatoa wasiwasi wakandarasi
ambao walikuwa wanaidai serikali kwa kusema tatizo hilo ni la mda mfupi kwani
serikali ya awamu ya tano itahakikisha inalimaliza tatizohilo.
“Ninachowaomba ondeeni wasi wasi kuhusu madeni haya
ya wakandarasi kwani kwa sasa mmeona waote jinsi serikali ya awamu ya tano
ilivyovunja katika kukusanya kodi tumeshuhudia tumepata zaidi ya trioni 1.4 kwa
mwenzi,kwahiyo tunauwezo wa kuyalipa madeni yote”
Katika hatua nyengine Waziri Mbarawa alifanya ziara
katika ujenzi wa upanuzi wa barabara kutoka mwenge jijini dar es salaam hadi
Morocco jijini hapa,huku waziri huyo
akifurahishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo kwenda kwa kasi kubwa,
Barabara hiyo ambayo imejengwa kutokana na fedha
zilizotakiwa zitumike kwenye shuhuri ya kusherekea uhuru ya tehere 9 Desemba
ambao Rais Magufuli alifuta sherehe hizo akiwataka Watanzania kujumuika kwenye
usafi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni