GAVANA WA BENKI KUU AWAONYA TRA,NI KUHUSU UKUNJAJI REKODI YA UKUSANYAJI WA KODI,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
Siku moja kupita baada ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA)
kutangaza kuvunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato nchini baada ya kusema
wamekusanya trioni 1.4 kwa mwezi Desemba,
Naye
Gavana wa Benki kuu nchini,Profesa Benno Ndulu amewatadhaharisha (TRA) kwa
kuwaambiawasizani kiwango hicho walichokusanya kuwa kinaweza kubaki hapo hapo au kuongezeka kwa
miezi hii ya mwanzo wa mwaka,
Kwa
madai kuwa miezi ambayo TRA wamekusanya kodi hiyo ni miezi ya mwisho wa mwaka ambayo makampuni mengi wanatumia miezi hiyo
kufanya majumuhisho.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jiji Dar es Salaam,Profesa Ndulu amesema hatua
waliyofikia TRA ya kuvunja rekodi ya ukusanyaji kodi ni nzuri ila amesema
katika kipindi hiki cha mwenzi wa pili,tatu na wa nne uwenda kiwango cha kodi kikapungua kwa madai miezi hii makampuni
hutumia kipindi hichi kujipanga upya.
“Kodi hii tuliyokusanya mwishoni mwaka jana kwa
kuvunja rekodi hii tusitegemee tena kama tutakusanya kwa miezi hii ya kwanza
kwani makampuni mengi hutumia miezi hii kujipanga upya,kwahiyo uwenda kiwango
cha kodi hichi kikapungua au kikabaki hapo hapo”amesema Profesa Ndulu.
Katika hatua Nyengine Profesa Ndulu amesema kitendo
cha TRA kuongeza ukusanyaji wa mapato hayo hakitaweza kusaidi thamani ya
shilingi yetu kuongezeka thamani huku akitaja njia ambazo zitasaidia thamani ya
pesa kitanzania kuongezeka.
Akizitaja njia hiyo ni kuongeza kuuza mauzo nje ya
nchi na ili iweze kusaidia kupata pesa nyingi za kigeni jambo analodai ndio
njia pekee itakayoweza kuongeza thamani ya fedha yetu,
Hakuna maoni
Chapisha Maoni