Zinazobamba

MAKAMU WA RAIS ATINGA KIZIMBANI,SOMA HAPA KUJUA

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Maalim Seif Shariff Hamad (mwenye suti ya kijivu)akiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo jijini Dar es Salaam, akisikiliza kesi inayomkabili wa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Liipumba na wenzake 30 wakituhumiwa kufanya mkusanyanyiko usio halali. (Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii).

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad leo amehudhuria katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba na wenzake 30 wa chama hicho.

       Maalimu Seif alifika na msafara wake wa magari matatu Mahakamani hapo  majira ya saa nne asubuhi.

       Hakimu wa Makakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Cyprian Mkeha amesema washitakiwa hao wanadaiwa kufanya kosa la jinai la kufanya mkusanyiko usio halali kwa mujibu wa sheria za nchi.

       Hakimu huyo ametoa dhamana kwa watu wote kutokana na maelezo yao kama masharti ya dhamana yalivyokuwa yakihitajika 

       Hakimu huyo, amesema kuwa  kesi inayomkabili Profesa Lipumba na wenzake 30 ni ya kufanya mkusanyiko usio halali kwa mujibu wa sharia za nchi mnamo januari 22 na 27 maeneo ya Temeke jijini Dar es Salaam na upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika.
         Jopo la mawakili wa kesi hiyo likiongozwa na Wakili,Job Karario awali walipeleka pingamizi la mashtaka dhidi ya Profesa Lipumba na wenzake 30.
      Hakimu  Cyprian aliahirisha kesi hiyo mpaka itakapotajwa tena Mei 6 mwaka huu na washitakiwa wote katika kesi hiyo wamepewa dhamana.
chanzo michuzi.blogs

No comments