Zinazobamba

Jamii imetakiwa kulinda na kutunza Mazingira ikiwemo vyanzo vya Maji ili kuepuka ukame.

Na Mussa Augustine.

Mkurugenzi Msaidizi huduma za ramani kutoka Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Elizabeth Mrema ameitaka jamii kulinda na kutunza Mazingira ikiwemo vyanzo vya  Maji ili kusaidia kuepukana na majanga mbalimbali yanayoweza kutokea ikiwemo hali ya ukame.
Mkurugenzi Msaidizi huduma za ramani kutoka Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Elizabeth Mrema.
Rai hiyo ameitoa Jijini Dar es salaam katika Washa  iliyohusisha watalaam wa Mazingira kutoka nchi wanachama wa  RCMRD ambao wamekutana kwa siku mbili kwa ajili ya kujadili mradi unaotumia teknolojia ya ramani kwa ajili ya kuangalia uharibifu wa vyanzo vya Maji.

Amesema kwamba mradi huo ni wakutumia satelaiti kupata taarifa za uchafuzi wa Mazingira ambapo umeanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2016 chini ya Shirika la Msaada la Marekani( USAID ),nakwamba umeonekana kuwa na manufaa makubwa kwa nchi za mashariki na kusini mwa Afrika.

"Tunashirikiana na kituo Cha RCMRD kilichopo nchini Kenya kwani Tanzania ni miongoni mwa  Nchi ishirini wanachama wa kituo hiki tangu mwaka 1975 ambapo kituo hiki kinatoa mafunzo yaliyojikita kwenye ardhi ikiwemo Maji,ardhi  ,milima pamoja na Misitu" amesema Elizabeth.

Kupitia Washa hiyo ya siku mbili itasaidia kubaini changamoto zilizojitokeza kwenye utekelezaji wa mradi huo wa majaribio nakutoa ushauri kwa viongozi wanaohusika katika utunzaji wa rasilimari za kwenye ardhi ikiwemo vyanzo vya asili vya Maji.
Kenneth Kasera kutoka RCMRD.
Kwa upande wake Kenneth kasera kutoka RCMRD amesema kwamba lengo na madhumini yakufanyia washa hiyo hapa nchini nikuonyesha kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama wa kituo hicho waliobahatika kupata mradi wa majaribio utakaokua na manufaa makubwa kwa wananchi wake.

"Ramani na picha tulizofanyia utafiti wa mradi huu wa majaribio uliodumu kwa miaka sita sasa  tutazionyesha nakuzijadili kwa pamoja ili tutoke na maadhimio ya pamoja yakwenda kuzishauri Serikali zetu nini kifanyike ili masuala mbalimbali ya ardhi ikiwemo vyanzo vya Maji  viweze kutunzwa" amesisitiza Keneth
Calvin's Wara kutoka RCMRD
Nae Calvin's Wara kutoka RCMRD upande wa Masuala ya  Adhi amesema kwamba tayari wameshafanya majaribio katika Mto rufiji,Ziwa Chald na maeneo mengine nakubaini changamoto zinazopelekea uharibifu wa rasilimali zilizopo kwenye ardhi na kusaidia kupata ufumbuzi wake.



Hakuna maoni