WAMACHINGA MWANZA WAISOMA NAMBA KISAWA KISAWA,SOMA HAPO KUJUA
Watu tisa (9) wamejeruhiwa katika vurugu wakati wa
kuwaondoa wafanyabiashara wadogowadogo sehemu zisizo ruhusiwa wilayani
Nyamagana, mkoani Mwanza
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa w Mwanza DCP Ahmed
Msangi imesema kwamba tukio hilo limetokea mnamo tarehe 05.03.2017 majira ya
saa15:45hrs katika mtaa wa Buhongwa Center ambapo watu tisa wakiwemo askari
mgambo wa jiji la mwanza saba (07), afisa mazingira mmoja (01) na dereva wa
jiji mmoja (01) walijeruhiwa.
Amesema watu hao walijeruhiwa kwa kupigwa na mawe
sehemu mbalimbali ya miili yao na wafanyabiashara wadogowadogo waliokuwa
wakifanya biashara pembeni ya barabara wakishirikiana na watu wengine waliokua
wakishabikia wakati wakiendelea na zoezi la kuwaondoa wafanya biashara
wadogowadogo katika maeneo yasiyo ruhusiwa haswa kwenye hifadhi ya barabara ya
mwanza kwenda shinyanga.
Aidha, Msangi amesema katika harakati za kudhibiti
vurugu hizo askari walifanikiwa kuwakamata watu tisa ambao inadaiwa kuwa
walikuwa wakihusika katika vurugu hizo kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi
utakapokamilika, watafikishwa mahakamani.
Majeruhi wote wapo hospitali ya mkoa ya Sekou Toure
wakiendelea kupatiwa matibabu na hali zao inaendelea vizuri.