Zinazobamba

SAKATA LA MAKONDA KUITEKA KITUO CHA CLAUDS,WAZIRI NAPE AUNDA TUME YA KUCHUNGUZA,SOMA HAPO KUJUA



Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ameunda kamati ya kuchunguza kuhusu tukio lililofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kutaka apewe matokeo ndani ya saa 24.

Nape ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari  mara baada ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uaandaji wa Clouds Media Groups, Ruge Mutahaba kuthibitisha kuwa Makonda alivamia kituo hicho, Ujumaa usiku akiwa na polisi wenye silaha.

“Matukio kama haya hutokea pindi nchi inapotaka kupinduliwa, lakini kama Rais yupo na nchi haijapinduliwa  basi kuingia ndani ya chombo cha habari na silaha, huku ni sawa na kunajisi uhuru wa habari.

"Kabla ya kuchukua hatua zozote, sisi kama Serikali tunataka kusikia kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

"Tumeunda timu ya watu 5 kufanya kazi katika saa 24 ili wapate maelezo ya RC Makonda na ripoti hiyo itasomwa wazi

"Kitendo kilichofanywa na RC Makonda kinanajisi Uhuru wa Vyombo vya Habari katika Nchi Huru. Mamlaka zitajua cha kufanya

"Wanahabari tutulie na tusubiri kusikia kutoka pande zote mbili kabla ya kuchukua uamuzi

"Natoa pole kwa Clouds Media na kwakuwa tumejiridhisha kuwa jambo hili limetokea basi tutalishughulikia

"Ripoti itakayoletwa na Kamati ya Uchunguzi pamoja na hatua zitakazochukuliwa vitatangazwa hadharani baada ya saa 24." Amesema Waziri Nape