Raisi Magufuli: Hata mkeo anaweza asikupende siku nyingine, cha muhimu ni kuchapa kazi
Rais Magufuli leo mkoani Mtwara wakati akiweka jiwe
la msingi katika kituo cha kupooza umeme njia ya KV 132 amelipongeza Shirika la
Umeme nchini Tanesco na kumpongeza Waziri wa Nishati na Madini, kwa juhudi zake
katika kazi.
Rais Magufuli amesema aliamua kumteua Sospeter
Muhongo kuwa Waziri kutokana na ukweli kwamba alikuwa anaona uchapaji wake wa
kazi kipindi ambacho yeye ni Waziri wa Ujenzi.
"Lengo lililokuwa kwenye ilani ya
Uchaguzi kwa mwaka jana ilikuwa asilimia thelathini na kitu nyinyi mkafika mpka
asilimia arobaini, na sasa hivi mko zaidi ya asilimia 46 sasa nisipowapongeza
nitakuwa mtu mbaya wa moyo mbaya.
" Na mimi na moyo mzuri kweli ndiyo maana nawapongeza wizara pamoja na Tanesco haya matatizo mengine ambayo yanatokea ni kwa sababu tuliingia mikataba ya hovyo huko nyuma, ya kulipia capacity charges ninajua mnayashughulikia na tunajaribu kutafuta pesa za mikopo tulipe haya madeni twende na Tanesco mpya" alisema Rais Magufuli

Mbali na hilo Rais Magufuli alimsihi Waziri wa
Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo
"Nilipoteuliwa kuwa Rais sikuona
mtu mwingine anayefaa kama Muhongo, nikamrudisha hapa hapa sababu mimi
nilipokuwa nikihesabu kilometa za barabara yeye alikuwa anaesabu kilometa za
nyaya, kwa hiyo nilifahamu kazi yake na saa zingine ukifanya kazi vizuri
unakuwa kama hupendwi pendwi hivi, lakini kwa nini wakupende? Hata mke wako
anaweza asikupende siku zingine, wewe chapa kazi" alisisitiza
Rais Magufuli
Rais Magufuli aliendelea kusisitiza kuwa katika
maisha ya kila siku huwezi kupendwa na kila mtu
"Hata ndugu yako anaweza
asikupende, saa zingine hata baba yako au hata mdogo wako anaweza asikupende,
huwezi ukapendwa na kila mmoja, hata mitume hawakupendwa na wote na wengine
walisulubiwa pamoja na kwamba walifanya mazuri.
"Kwa hiyo Prof. Muhongo wewe fanyakazi tena usihangaike hata kusoma ile mitandao, mimi sisomagi hiyo mitandao achana nayo watandae huko huko wenyewe wewe chapa kazi" alisisitiza Mhe. Rais Magufuli.
"Kwa hiyo Prof. Muhongo wewe fanyakazi tena usihangaike hata kusoma ile mitandao, mimi sisomagi hiyo mitandao achana nayo watandae huko huko wenyewe wewe chapa kazi" alisisitiza Mhe. Rais Magufuli.