KUBWA LEO-TUNDU LISSU ADAKWA TENA NA POLISI,SOMA HAPO KUJUA
Jeshi la Polisi nchini linamshikilia Mbunge wa
Singida Mashariki, Tundu Lissu baada ya kuachiwa huru na Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu.
Lissu aliachiwa leo asubuhi na Hakimu Mkuu Mkazi,
Huruma Shahidi baada ya upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Paul Kadushi
kuwasilisha hati ya kuondoa shtaka hilo.
Kadushi aliwasilisha hati hiyo chini ya kifungua
namba91 (1) cha makosa ya jinai akionyesha DPP hana haja ya kuendelea na kesi,
mahakama ikaridhia na kumuachia.
Muda mfupi baada ya kuachiwa na kutoka nje ya
mahakama alikamatwa tena na askari waliokuwapo mahakamani hapo na kupelekwa
Kituo Kikuu cha Polisi.
Lissu alikuwa anashtakiwa kwamba Januari 11, mwaka
huu katika kampeni za uchaguzi jimbo la Dimani aliwashawishi watu wasiridhike
na wawe na nia ovu dhidi ya utawala.