FREEMAN MBOWE AMGOMEA MAKONDA,APIGILIA MSUMARI ASEMA YEYE SI WA KUITWA KAMA "MHUDUMU WA BAA"SOMA HAPO KUJUA

Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikaeli Mbowe amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda hana mamlaka ya kumuita kwenda Kituo cha Polisi.
Mbowe ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari Mjini Dodoma kufuatia kutajwa katika orodha ya watuhumiwa
65 wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kutakiwa kufika Kituo cha
Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam leo saa tano asubuhi.
Mbowe amekanusha vikali tuhuma hizo za kujihusisha
na biashara ya dawa za kulevya na kusema kuwa anachokifanya RC Makonda ni
kuwaepusha watuhumiwa wa kweli wa dawa za kulevya na mikononi mwa sheria.
Aidha, Mbowe amesema kuwa yupo tayari kutoa
ushirikiano kwa Jeshi la Polisi muda wowote endapo njia sahihi
zitakapofuatwa.
Pia amesema atamfungulia mashtaka RC Paul Makonda
kwa kumchafulia jina lake kufuatia kumtuhumu kwa biashara ya dawa za kulevya.
Kiongozi huyo wa Kambi ya Upinzani Bungeni amesema
kuwa wao hawana ugomvi wowote na Jamhuri bali Paul Makonda binafsi.
Wakati huo huo, Kiongozi wa Upinzani Bungeni na
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa jimbo la
Hai, Freeman Mbowe amekutana na kufanya mazungumzo na Wabunge kutoka
Bunge la Ulaya, David Martin, Gerrard Quille, Balozi wa Umoja wa Ulaya
Tanzania, Roeland Van De Beer na Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje,
Afrika Mashariki na Kikanda,Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, mjini Dodoma
leo Ijumaa 10/02/2017