DC HAPI AWASIHI WATENDAJI KINONDONI,NI KUHUSU FEDHA ZA MIRADI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani aliyevaa suti ni MKuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi akisikiliza kero kutoka kwa wananchi wakati alipokuwa kwenye ziara zake kwenye kata 10 ndani ya Manispaa hiyo kwa lengo la kukagua mipango ya maendeleo pamoja na kuwasikiliza kero wananchi |
NA
KAROLI VINSENT
Mkuu
wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi amewataka
watendaji wa kata kuzisimamia fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya
miradi maendeleo ili kuweza kuziokoa fedha hizo kupotea.
Pia,Hapi
amewaagiza watendaji hao kuhakikisha fedha inayotenga kwenye mradi husika
ilingane na thamani harisi ya fedha.
Mkuu
huyo Wilaya ,ameyasema hayo leo Wakati alipokuwa kwenye ziara katika Kata ya
Bunju ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya Siku 10 ,ziara hiyo yenye lengo la
kukagua miradi ya Maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
Amesema
nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha fedha za serikali hazipotei
hivyo anawahimiza watendaji wa serikali za mitaa kuhakikisha wanasimamia fedha
zilizotengwa kwenye miradi.
"Hizi
milioni 700 mlizopewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo hakikisheni mnazitumia
kwa uangalifu na umakini ili zisipotee hovyo,hata hiyo miradi ya maendeleo
inayojengwa ilingane na thamani ya fedha"amesema Hapi.
Amesema
kuna baadhi miradi inayotekelezwa hailingani na thamani ya fedha iliyotengwa
jambo analozidi wahimiza kusimamia kwa umakini fedha.
Hata
hivyo,Hapi amewata watendaji wa kata kuhakikisha wanayaweka maeneo hayo kwenye
mipango (master Planning) ili kuweza kuyabaini maneo ya wazi katika eneo
husika.
"Ninavyoka
kila kata kuwa master Planning lengo ni kutaka kujua maeneo yapi ya wazi
yalivamiwa ,maana kwa sasa Kinondoni,hatutaki kuwa kama wenzetu huku nyuma
ambao waliruhusu maeneo ya wazi kuvamiwa,nataka niwahakikisha kwa sasa sisi
tutakuwa wakali sana kwenye maeneo ya wazi yaliyochukuliwa na watu ili yaweze
kurudi,”amesema Hapi.