ASKOFU GWAJIMA NA BILIONEA MANJI WAENDELEA KUSOTA SELO,SOMA HAPO KUJUA

Kamanda Sirro amesema bado wanamshikilia
mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji pamoja Askofu wa kanisa la Ufunuo na Uzima,
Josephat Gwajima kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya na
upelelezi dhidi yao bado haujakamilika.
Watuhumiwa hao wawili waliripoti kituoni hapo jana
mchana na siyo leo kama walivyoagizwa na RC Paul Makonda.
Kamanda Sirro amesema atatoa taarifa Jumatatu
kueleza nini kinaendelea kuhusu watuhumiwa hao.
Mpaka wakati anazungumza na waandishi wa habari
kamanda huyo alisema walioripoti kituoni hapo ni watuhumiwa 4 kati ya 65 .
Walioshuhudiwa na waandishi wa habari wakiripoti
kituoni hapo ni Iddi Azzan, Hussain Pamba Kali pamoja na bosi Sea Cliff.