ACT-WAZALENDO YAJITOSA KUMTETEA MBOWE,ZITTO KABWE AMRUSHIA KOMBORA MAKONDA,SOMA HAPO KUJUA

Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye pia ni Kiongozi wa
Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amemkingia kifua Mwenyekiti wa CHADEMA
Freeman Mbowe na kusema kuwa anaamini Mbunge huyo wa Hai hajawahi kujihusisha
na dawa za kuleva kwa namna yoyote
Zitto ambaye ameambatana na Mbowe katika mkutano
wake na wanahabari leo mjini Dodoma, amesema kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Paul Makonda kumtaja Mbowe katika sakata la dawa za kulevya ni
sawa na kutangaza vita na chuki dhidi ya chama hicho.
Amesema kuichafua CHADEMA ni sawa na kuuchafua
upinzani hivyo na yeye hawezi kukaa kimya kuona upinzani ukishambuliwa, na
ndiyo sababu ya kuongeza nguvu kwa kuungana naye.