Zinazobamba

RAIS MAGUFULI KULILIZA KANISA KATOLIKI NCHINI,AGIZO LAKE KUVIMALIZA VYUO VYA KANISA HILO,SOMA HAPO KUJUA



http://i0.wp.com/mtembezi.com/wp-content/uploads/2016/09/magufuli-magomeni.jpg?resize=497%2C297
RAIS John Magufuli agizo lake la kutaka orodha ya vyuo vikuu nchini iangaliwe  upya huku akitoa maelekezo ya kutaka kubakiwa na  vyuo vikuu vichache vyenye sifa,sasa agizo hilo linatajwa uwenda likaliweka pabaya Kanisa Katoliki nchini ambalo ndio linatajwa kumiliki vyuo vikuu vingi.(Mtandao huu umeelezwa).Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Rais Magufuli  mara kwa mara amekuwa akiitaka Tume vya Vyuo Vikuu nchini (TCU) kuangalia na kupunguza wingi wa vyuo vikuu nchini kwa kile anachokisema vyuo vikuu vingi vimeanzishwa huku vikiwa havina sifa ya kuwa vyuo vikuu.

Pamoja na hayo Rais Magufuli alielekeza TCU kuangalia na kuhakikisha wanabakiza vyuo vikuu vichache huku akivitaja kwa majina  vyuo vikuu hivyo ni chuo kikuu cha Mliman na chuo kikuu cha Dodoma kwa kile anachodai kinanafasi ya kuchukua wanafunzi wote wanaohitajika kuingia chuo kikuu.


Baada ya Agizo hilo la Rais,linatajwa litaliweka pabaya Kanisa Katoliki kutokana na kutajwa kumiliki vyuo vikuu vingi sana nchini huku ikitafsiriwa agizo hilo uwenda likalilenga kanisa hilo.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu aliyoko ndani ya (TCU) ambaye hakutaka kutajwa jina lake mtandaoni,ameumbia mtandao wa (Fullhabari.blog) kuwa agizo hilo linaligusa moja kwa moja Kanisa Katoliki nchini ambapo linatajwa  kutajwa kumiliki vyuo vikuu vingi.
“Nichokwambia hili agizo lazima litaleta msuguano mkubwa,yaani  kanisa Katoliki haliwezi kupona kabisa ndugu kwani linautilili wa vyuo vingi sana,hata Magufuli anavyosema vyuo vya (St nan) vingi vinamilikiwa na Kanisa Katoliki pamoja na Madhehebu mengine,yaani nakuhakikisha lazima vifungwe tu maana mkubwa kaamua sisi tufanyaje?”amehoji mtoa taarifa wetu huyo.

Uchunguzi uliofanywa na Fullhabari.blogs umebaini Kanisa Katoliki linatajwa kumiliki vyuo vikuu vya Mtakatifu Jordan cha Morogoro,Chuo kikuu cha Mwenge,Chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino,chuo kikuu cha  mtakatifu Joseph,Chuo kikuu cha sayansi cha Mwanza pamoja na kutoa  matawi mengi ya Vyuo vikuu kutumia mwavuli wa Chuo Kikuu cha Mtatifu Augustino,

‘”Yaani kwa mfano  chuo cha Mtatifu Jordan hiki hakiwezi kupona hata katika kukipandisha hazi kwake kilikuwa na utata,leo chuo cha Sauti kimekuwa na matawi mengi mengine hayana hata hadhi ya kuwa matawi,yaani nakuhakikishia,lazima kilio kitakuja tu wewe ngojea”kimesema chanzo chetu.

Mbali na Kanisa katoliki pigo hilo linatajwa pia kuyagusa madhehebu mengine ambayo nayo yanatajwa kuhusika katika kuanzisha utilili wa vyuo vikuu ambavyo hata kuanzishwa kwa kulikuwa na utata.