Zinazobamba

AJIRA MPYA ZA WALIMU ZAIPASUA SERIKALI YA JPM,NAIBU WAZIRI WAKE AAMUA KUFUNGUKA UKWELI UWEPO WA AJIRA HIZO,SOMA HAPO KUJUA

Naibu Waziri ofisi ya Nchini,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)Suleiman Jaffo (kulia)akizungumza na Mwandishi wa Fullhabari.blogs Karoli Vinsent (Kushoto)(Picha na Maktaba)


KILE kinachoonekana kuwa Ajira za Walimu wapya ni kama zimeanza kuipasua serikali ya awamu ya Tano,baada ya Viongozi wa wakuu hususani Mawaziri kushindwa kutaja tarehe ya lini serikali itaanza kuajiri walimu hao wapya,ambapo sasa Viongozi hao wamefunguka na kusema  Rais John Magufuli ndio mwenye sauti ya mwisho kwenye ajira hizo.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo

Hayo yamebainishwa  Jana Jinini Dar es Salaam na  Naibu  Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Suleiman Jaffo wakati alipokuwa anaongea na (Fullhabari.blog) ambapo Waziri huyo alisema kwa sasa suala la ajira za walimu lipo kwa Rais John Magufuli ndio atakapoamua lini zitatoka.

Kauli hiyo Jaffo inakuwa mara baada ya Mwandishi wa Mtandao huu alipomtaka ataje tarehe lini serikali itatangaza ajira hizo,alisema serikali ilitakiwa kuajiri walimu elfu 35 ambapo amedai zoezi hilo lilisitishwa kutokana kupisha uhakiki wa watumishi hewa.


“Ni kweli tutaajiri walimu ila kama mlimsikia Rais Magufuli wakati alipokuwa anaongea na waandishi wa habari,alisema serikali imeanza kuajiri ,na kwa kuanzia wameanza katika chuo cha Mloganzira,ila nakuhakikisha yeye ndio mwenye Mamlaka hata katika hizo za ajira za walimu wapya,”alisema Waziri Jaffo.

Waziri Jaffo alisema serikali inampango wa kuajiri walimu waliomaliza vyuo mwaka jana (2015) na mwaka huu (2016) huki akibanisha kuwa kwa sasa nchi inauhaba  wa walimu wa sayansi na hata katika ajira hizo eflu 35 wataangaliwa walimu watapewa kipaumbele.

Kauli hiyo Jaffo inakuja ikiwa ni baada ya Viongozi wa Chama cha Walimu nchi(CWT) wakiitaka serikali ya Magufuli iseme ukweli kuhusu ukweli wa ajira hizo kama zipo au hazipo,kwa kile wanachokida kuwa serikali  haina fedha za kaujiri walimu hao na imeamua kijificha kwenye kichaka cha "Watumishi hewa".

Akihojiwa na Gazeti la Tanzania Daima mwanzoni mwa hiki hii,Katibu Mkuu wa (CWT), Ezekiah Oluoch alisema inasikitisha serikali kutokuwa na jibu kamili za ajira hizo kwa kile anachokisema zoezi gani la uhakiki lisilo kwisha.

“Wasema Ukweli kama shida ni fedha hakuna za kuajiri watumishi hao,zoezi la kuhakiki gani mpaka sahivi,maana shule hazina walimu,ziko shule zinamwalimu mkuu tu ndio anafundisha peke yake,leo walimu wamehitimu wapo mtaani na serikali inashindwa kujairi kwa hoja ya watumishi hewa”alisema Oluoch.

Sakata la Ajira mpya za Walimu zilianza kuwa ngumu pale Rais Magufuli Juni mwaka huu alipotangaza kusitisha ajira mpya zote serikali kwa madai kuwa serikali inahakiki watumishi hewa,na kuahidi zoezi la hilo litaisha ndani mwezi mmoja na nusu baada ya hapo ajira hizo zitaanza kutolewa.

Ambapo sasa miezi takribani mitano imepita baada ya Zuio hilo la Rais Magufuli kupita na hakuna hata ajira hizo za Walimu huku bado kukiwa na mahitaji makubwa ya awalimu katika shule za Msingi na Sekondali nchini,

Na inaleezwa kuwa Takribani ya wahitimu ya uwali wa mwaka 2015 na wa mwaka huu wakiwa wamemaliza mafunzo hayo,huku ikikadiliwa walimu hao wanafikia zaidi ya elfu 80.