Zinazobamba

SAKATA LA DANGOTE KUFUNGA KIWANDA CHAKE,SHIRIKA LA TPDC LAIBUKA NA KUSEMA HAYA,SOMA HAPO KUJUA

http://www.tpdc-tz.com/assets/img/logo1-red.png
NA KAROLI VINSENT
HUKU kukiwa kuna taarifa kiwanda cha uzarishaji na uuzaji saruji cha (Dangote)kilichopo mkoani  Mtwara kitangaza kusitisha uzarishaji wa saruji hiyo kwa kile inachoelezwa  kuwa shirika la Maendeleo  ya Petroli nchini (TPDC)limeshindwa kuwauzia gesi asilia kwa bei rahisi kwenye kiwanda hicho.

Nalo,Shirika la TPDC limeibuka na kukunanusha taarifa hiyo na kusema shirika hilo limefanya jitihada mbali mbali za kuhakisha kiwanda cha Dangote kinapata nishati ya gesi.

Pia shirika hilo limesema limekuwa likifanya vikao mbali mbali na kufanya makubaliano yaliofanyika baina yao na mwekezaji huyo ili kuhakikisha  wanaridhia nia yao ya kutumia gesi asilia ya kuzalisha umeme kwa ajili ya kiwanda cha sajuri ambacho kipo Mkoani Mtwara ambacho kinatajwa kuajiri watanzania wengi.


Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,Kaimu wa nisharti na Madini,John Shija  amesema TPDC hufuata kanuni na utaratibu wa kupanga bei ya gesi asilia ambapo hupanga kulingana na aina ya mteja ,huku akidai wateja wamegawanyika kufuatia makundi tofauti kama vile wateja wa viwandani,majumbani,magari pamoja na wateja  wa kuzalisha umeme.

Ameeleza kuwa hata hoja bei ya gesi asilia,huwa  inapendekezwa na TPDC  lazima iridhiwe na ipitishwe na EWURA ndipo ianze kutumika.

“Dangote kama mtumiaji wa matumizi ya  viwandani amekuwa na mazungumzo na sisi kwa mdamrefu kuhusu bei ya gesi asilia,na hiko kiwanda kimeomba kupewa gesi asilia kwa bei ambayo hapa kwetu Tanzania ni kidogo kwani kiasi hicho cha bei ndicho kinacholipwa kununuliwa gesi ghafi kutoka kiwandani”amesema Shija.

Hata Hivyo,Shija amesema shirika hilo limeshafanya  mikataba ya awali na kiwanda hicho kwa ajili ya kuwauzia gesi asilia itakayotumika kuzalishia umeme utakuwa unatumika katika kiwanda cha Dangote.

Huku akidai kuwa mpaka mwezi January 2017 miundombinu ya gesi asilia itakuwa imeunganisha na mitambo ya kufua umeme utakaotumiwa na kiwanda hicho.

Shija amesema shirika la mafuta ya Taifa limekuwa linafanya kazi zake kwa kufauata sheria ,kanuni na taratibu za nchi,pamoja na kuwajali  wawekezaji akiwemo Dangote ili wawekezi katika kukuza uchumi wa nchi.

Pamoja na hayo,Shija ameitaka jamii kuacha kuzusha taarifa ambazo hazina mantiki.