Zinazobamba

WADAU WATOA MAONI TOFAUTI KUHUSU ADHABU YA KIFO...


Wadau kutoka Asasi mbalimbali za kiraia nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu nchini, Bahame Tom Nyanduga (Wa pili kutoka kulia waliokaa) pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini (wa pili kutoka kushoto waliokaa) Bw. Roeland Van De Geer wakati wa kongamano la kujadili adhabu ya kifo. Kongamano hilo liliandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu.

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha sheria na haki za Binadamu nchini Tanzania Bi Hellen Kijo Bisimba Akichangioa mada katika mjadala wa waazi uliofanyika Jana Jijini Dar es salaam kujadili kwa Pamoja Uwepo au kutokuwepo kwa Adhabu ya Kifo.

Katika Mjadala Huo Bi Hellen Kijo Bisima ameeleza kuwa Ahabu ya kifo ni moja kati ya adhabu ambazo hazina lengo la kuRekebisha Tabia ya mtenda kosa bali imekuwa kama ni kisasi kwa Mtenda kosa hivyo pamoja na kwamba haitekelezwi nchini  Tanzania bali pia inafaa kuondolewa kabisa katika Sheria za nchini kama kama mattaifa kadhaa ya africa yalivyochukua uamuzi wa kufuta adhabu hiyo.

Aidha amesema kuwa kuendelea kuwawepo kwa wahukumiwa wa adhabu hiyo na kuendelea kuwepo magerezani wakisubiri kunyongwa lakini Hawanyongwi ni kuendelea kuwatesa wafungwa hao kuakili na kuwafanya waishi kwa wasiwasi kwa kuwa hawajui ni lini adhabu hiyo itatekelezwa kwao.

Lhrc wameiomba serikali kufanya mchakato wa kuangalia uwezekano wa kuondoa kabisa sgeria hiyo kwani pamoja na kwamba inakiuka haki ya binadamu ya kuishi bali pia ni sheria ambayo haikutungwa na watanzania ni sheria ambayo imetungwa enzi za wakoloni na sisi tukaitumia kama tulivyoikuta.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Bw. Roeland Van De Geer  akitoa maoni yake katika Mjadala huo wa Kujadili kwa pamoja na wadau juu ya  Hukumu ya adhabu ya kifo nchini Tanzania ambapo balozi hyu amesema kuwa huu ni wakati sasa wa Tanzania kuangalia upya sheria hii na kupima kama inafaaa kuensdelea kuwepo nchini kwetu au inafaa kufutwa kama maiaifa mengi yalivyoifuta hivi karibuni.

Kaimu Mkurugenzi wa LHRC Bi IMELDA LULU URIO akiendesha majadiliano hayo ambayo yalifanyika katika ukumbi wa British council Jijini Dar es salaam  jana kujadili pamoja na wadau juu ya adhabu ya kifo na uwepo wake nchini Tanzania.



Licha ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokeleza adhabu ya kifo kwa zaidi ya miaka 20. Imeendelea kusisitizwa kuifuta sheria ya adhabu ya kifo kwa watuhumiwa wa makosa ya mauaji kwa kuwa haisaidii kupunguza makosa hayo na kwamba iangalie chanzo cha tatizo hilo kwa lengo la kufanyia marekebisho.
Ushauri huo umetolewa leo na wadau mbalimbali wa haki za binadamu katika kongamano la kuijadili adhabu ya kifo nchini, lililoandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN).
Wadau hao wamesema kuwa, falsafa ya ukuaji wa adhabu huzingatia vigezo viwili ambavyo ni kutoa funzo kwa jamii pamoja ma kumrekebisha mkosaji. Wadau hao wameitumia hoja hiyo kuisisitiza serikali kufuta adhabu ya kifo kwa kuwa endapo mtuhumiwa akiuawa hatopata fundisho na pia kifo chake kinatafsiriwa sawa na kosa hilo kujirudia.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Hellen Kijo-Bisimba amesema kituo hicho hakitaacha kuishauri serikali kuifuta adhabu hiyo kwa kuwa haisaidii kutokomeza matukio ya mauaji na pia huenda ikaathiri watu wasio na hatia.
“Inabidi serikali iangalie chimbuko la matukio ya mauaji ili litokomezwe na si kuhukumu watu kwa adhabu ya kifo, hatumaanishi wasihukumiwe bali watafutiwe adhabu nyingine kwa kuwa tangu kuanza kutumika adhabu hii matendo ya mauaji hayajapungua,” amesema.
Ameongeza kuwa ” Kumuua mtu si suluhisho bali kosa hilo linazidi kufanyika na si sahihi. LHRC tunaendelea kuipinga adhabu hii sababu haisaidii kupunguza mauaji,”
Bisimba amedai kuwa, asilimia kubwa ya wanaohukumiwa adhabu ya kifo ni watu wasio na kipato na kwamba hali hii huonyesha adhabu hiyo hutekelezwa kitabaka zaidi.
Mwakilishi wa UN, Roeland Van de Geev amesema kuwa shirika hilo halitailazimisha serikali kuifuta sheria hiyo bali litawezesha mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s) yanayohusika na haki za binadamu nchini kuishauri serikali kufuta adhabu hiyo.
“Nchi zaidi ya 140 duniani zimefuta adhabu hiyo, na hakuna matukio ya kutisha ya mauaji katika nchi husika, mfano Marekani inatekeleza adhabu ya kifo lakini matukio ya mauaji bado yanaendelea. Hii inamaanisha kwamba suluhu pekee ni kutibu au kuzuia vyanzo vya matukio hayo,” amesema.
Ameshauri kuwa “Adhabu hii hafai kutekelezwa sababu inaondoa utu wa mtu. Tanzania pamoja na nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki zifute sheria hiyo.”
Bahame Tom Nyanduga kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora amesema adhabu hiyo haistahili kuendelea kutekelezwa nchini kutokana kwamba ilianzishwa na wakoloni kwa lengo la kulinda utawala wao.
“Haki ya binadamu ya kuishi ndiyo msingi wa haki nyingine, katiba ya 1977 inatambua haki ya kuishi. Mahakama haiwezi futa adhabu hii bali serikali ndiyo yenye wajibu wa kuifuta sheria hiyo hivyo ni vyema ikafanya hivyo,” amesema.
Amesema ingawa serikali haijatekeleza adhabu hiyo kwa zaidi ya miaka 20 lakini inawajibu wa kuifuta sababu watu wanazidi kuhukumiwa.
“Nchi zaidi ya 20 Afrika zimefuta adhabu hii na hatusikii kama kuna kukithiri kwa matukio ya mauaji.Ni vigumu kuhusisha adhabu ya kifo kama suluhisho pekee la kutokomeza mauaji,” amesema.
Sheikh Ally Hemko kutoka Baraza Kuu la Waisilamu Tanzania (Bakwata) ameshauri jamii kuepukana na vitendo vya mauaji kwa kuwa dini hairuhusu.
“Dini yetu hufundisha kuwa mtu anayeua nae aue ingawa pia inasisitiza kuua ni dhambi hivyo ili kuondokana na utata huo, jamii inawajibu wa kuacha votendo hivyo sababu hata kama sheria hiyo ikifutwa watu wasio wema watazidi kuua,” amesema.