Zinazobamba

TAARIFA MUHIMU KUHUSU KUVUNJWA BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA TEMEKE,SOMAHAPO KUJUA

Kufuatia kugawana kwa mali na watumishi kwa Wilaya za Kigamboni na Temeke, hatimaye Baraza la Madiwani lililokuwa linaziunganisha halmashauri hizo limevunjwa, huku Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Temeke Abdallah Chaurembo akisisitiza mambo kadha wa kadha.baraza-tmk-4

Akizungumza katika kikao hicho cha kuvunja baraza Mstahiki Meya Chaurembo amewataka madiwani kusimamia vyema mapato na matumizi katika halmashauri watakazokuwepo ili zisije kuvunjwa kwani Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza kuwa halmashauri isiyokusanya mapato kuanzia asilimia 80 itafutwa.baraza-tmk-2

Pia amesisitiza kuwa bajeti ya bilioni 50 iliyotengwa huku bilioni 42 kwa Temeke na bilioni 8 kwa Kigamboni zitumike kama ilivyoagizwa na kuhakikisha kuwa inagusa maisha ya watu kwa kuboresha maisha huduma za jamii, halikadhalika miradi iliyopo Wilayani Temeke na ya Kigamboni itekelezwe kwenye wilaya husika na ikitokea kuna mgongano wa kimaslahi kuundwe kamati ya pamoja kujadili suala hilo.baraza-tmk-1

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amewataka madiwani hao kutatua kero za wakazi wao na kuwataka watenge siku za kusikiliza kero za wananchi wao na kuwaomba kusimamia watumishi kwenye suala la utoaji huduma na kuahidi kushirikiana na mkuu wa wilaya ya Kigamboni katika suala la ulinzi na usalama.