Zinazobamba

KITUO CHA SHERIA WAAZIMISHA MIAKA 21 YA KUANZISHWA KWAO KWA KUWAFARIJI WATOTO WENYE SHIDA...CHATIMIZA MIAKA 21


Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania LHRC akimkabidhi zawadi  mmoja wa watoto ambao wanalelewa katika Kituo cha makao ya Taifa ya watoto wenye shida kilichopo Kurasini Jjini Dar es salaam leo. 
Baadhi ya Vifaa mbalimbali vilivyotolewa na LHRC kwa watoto hao.  

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha sheria na haki za Binadamu LHRC akimkabidhi zawadi mbalimbali Afisa mfawidhi wa makao ya Taifa ya watoto wenye shida huko kurasin.
Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) kimeazimisha miaka 21 ya kituo hicho kwa kuwafariji na kuwakumbuka watoto wenye shida kwa kuwapeleka zawadi kadhaa zikiwamo sukari katika kituo cha makao ya Taifa ya watoto wenye shida kilichopo kurasini Jijini Daresalaam.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi zawadi hizo kwa afisa mfawidhi wa kituo hicho Beatrice Laurence, Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho Bi Kijo Bisimba amesema kumekuwepo na ukiukwaji wa haki za watoto katika jamii ya leo jambo linalosababisha kuwepo na watoto wa mitaani.
 
Amesema hali ya kutothaminiwa kwa haki za watoto zimendelea kuwa tatizo, kumekuwepo kwa ongezeko la watoto wa mitaani kwa sababu migogoro ya ndani ya familia wanazotoka, kupigwa, unyanyasaji na ukatili, uzalilishaji wa kingono, watoto kutumika katika biashara haramu kama madawa ya kulevya imekuwa ni kero kubwa.
 
WAPENDEKEZA SHERIA KALI
 Katika hatua nyingine kituo hicho kimependekeza serikali kupitia wizara ya afya, ustawi wa jamii,jinsia, wazee na watoto ikishirikiana na wizara ya sheria na katiba kufanya mabadiliko ya sheria ya mtoto na kuweka mkazo malezi bora kwa mtoto ikiwemo kuweka kipengere cha adhabu kali kwa familia itakayoshindwa kutimiliza wajibu wake wa malezi\

Serikali, jamii na wadau zinawajibu wa kushirikiana pamoja kutoa elimu ya malezi ili kuepuka tatizo la mayatima na watoto wa mitaani
 
Watoto wanaoishi makao ya taifa ya watoto Kurasini Jijini Dar es salaam wakisikiliza kwa makini wakati viongozi wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC walipokuwa wanazungumza nao walipowatembelea kituoni kwao kusherehekea nao kuadhimisha miaka 21 ya LHRC ambapo watoto hao wamepata fursa ya kuzungumza na maafisa hao na kupokea zawadi mbalimbali kutoka kwao ikiwa ni ishara ya upendo kwa watoto hao




Upendo wa bibi ulioje! Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bi. Kijo Bisimba akimrisha keki mmoja wa watoto wa kituo hicho.(Picha zote na Exaud Mtei)