Zinazobamba

GAVANA WA BENKI KUU AZUNGUMZIA TENA KUHUSU UCHUMI WA NCHI,SOMA HAPO KUJUA



 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh0skLfS4Bw8Z_SNjVH4aSyA2_di66q-3DDnZBU1ozy8zsrqP9MvxahWg_yVePob6-dhoisWsIqJnTtMDHMkd_IM3dDGeEoopgdnCYt3JNGpXAZoUvJZu8RLdibR1Jvaw02i5FhTy07if5f/s1600/3.JPG
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema ukuaji wa pato la Taifa umeongezeka kwa  asilimia 7.9 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 5.8 kwa kipindi kamahicho mwaka 2015.

Hayo yamebainishwa na Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu Dar es Salaam leo asubuhi wakati akizungumza na wanahabari kuhusu ukuaji wa pato la Taifa kwa robo na
nusu mwaka 2016.

Profesa Ndulu alisema shughuli za kiuchumi  zilizokua kwa kasi ya juu zaidi katika kipindi hicho ni usafirishaji na uhifadhi wa mizigo ikiwa ni asilimia 30.6, uchimbaji wa madini kwa
asilimia 20.5, mawasiliano na habari asilimia 12.6 na sekta ya fedha na  bima kwa asilimia 12.5.


Alisema ukuaji wa sekta ya uchukuzi na  uhifadhi wa mizigo umetokana na kuongezekea kwa usafirishaji wa abiria
kwa njia ya barabara na gesi asilia ambao umekua kwa zaidi ya nusu ukilinganisha na robo ya pili ya mwaka 2015 kwa asilimia 9.4.

"Kwa upande mwingine, ukuaji wa sekta ya uchimbaji wa madini na gesi umechangiwa zaidi na kuongezeka kwa uzalishaji wa gesi ambao umekua  kutoka mmSFt3.7,793 kwa mwaka 2015 mpaka mmSFt3 11,267 kwa mwaka 2016"
alisema Ndulu

Profesa Ndulu alitaja sekta nyingine ambayo  imefanya vizuri ililinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka 2015 kuwa
ni sekta ya kilimo ambayo imekua kwa asilimia 3.2 kwa robo ya pili ya  mwaka 2016 wakati mwaka jana ilishuka kwa asilimia 1.9.

Aidha sekta ya fedha na bima imekua kwa asilimia 12.5 kwa robo ya pili ya  mwaka 2016 ikilinganishwa na asilimia 10.0 kwa robo ya pili ya mwaka  2015.

Akizungumzia ukuaji wa pato la Taifa alisema katika nusu ya
mwaka 2016 yaani Januari hadi Juni 2o16 kasi ya ukuaji wa pato la taifa imeongezeka na kufikia asilimia 6.7 ikilinganishwa na asilimia 5.7 kwa  nusu ya kwanza ya mwaka 2015