RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI HUU LEO,SOMA HAPO KUJUA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli leo tarehe 25 Agosti, 2016 amemteua Bw. Andrew Wilson Massawe
kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Kabla ya uteuzi huo Bw. Andrew Wilson Massawe
alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta katika Benki Kuu Tanzania (BOT).
Bw. Andrew Wilson Massawe anachukua nafasi
iliyoachwa wazi na Dkt. Modestus Francis Kipilimba ambaye ameteuliwa kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Uteuzi wa Bw. Andrew Wilson Massawe unaanza mara
moja.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
25 Agosti, 2016