Zinazobamba

MADIWANI WA MANISPAA YA TEMEKE WAJADILI HICHI LEO,SOMA HAPO KUJUA

Baraza la Madiwani ni moja ya chombo muhimu cha kutetea maslahi ya wananchi kupitia uwakilishi wa madiwani wao, na mabaraza mengi nchini yamekuwa yakichukua hatua mbalimbali pale wanapoona mambo yanaenda ndivyo sivyo kwa maslahi yasiyokuwa ya wananchi.ABDALAH Chaurembo Meya TMK

Ambapo siku ya leo katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Temeke chini ya Mstahiki Meya Abdalah Chaurembo, limezungumza masuala mengi yenye tija kwa Taifa ikiwemo suala la muwekezaji wa kiwanja cha Osterbay maarufu kama 3 Star ambaye aliingia mkataba tangu mwaka 2013 na kwa mujibu wa mkataba huo ilibidi eneo hilo liendelezwe  kwa kuwa kitega uchumi ambacho kitaliingizia pato Halmashauri lakini imekuwa ndivyo sivyo.MRADI DMDP TMK (9)

Akichangia suala hilo Naibu Mstahiki Meya Salum Feisal Hassan, ameeleza kuwa muwekezaji huyo amevunja mkataba hivyo hatua stahiki inabidi zichukuliwe kwani amekuwa kama dalali wa kutafuta wawekezaji wengine waliendeleze eneo hilo, badala ya yeye mwenyewe kuwa na uwezo binafsi wa kufanya hivyo kama mkataba unavyoeleza.ABDALLAH MTOLEA

Katika hatua nyingine Mbunge wa jimbo la Temeke ambaye anaingia kama mjumbe kwenye Baraza la Madiwani Abdallah Mtolea, amewataka madiwani kujifunza sheria na kanuni za mabaraza ya madiwani, ili kuleta maelewano yenye tija kwa Halmashauri hiyo, jambo ambalo Mstahiki Meya Chaurembo ameeleza kuwa limetengewa bajeti na zoezi la semina litaanza hivi karibuni