HATIMAYE VIONGOZI WA DINI WAOKOA JAHAZI HILI LA WAPINZANI,SASA WAFANIKIWA KUMALIZA MTEGO HUU,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
HATIMAYE viongozi wa dini nchini wameweza kutatua
mtego wa kwanza wa vyama vya Upinzani nchini,baada wa vyama hivyo
kukubali kurejea kwenye Bunge la Jamhuri wa Muungano na kushiriki vikao
vyake. vinavyotarajia kuanza hivi karibuni
Awali Wabunge wa upinzani walikataa kushirika vikao
vyote vya bunge hilo ambavyo vitaongozwa na Naibu Spika DK Tulia Acksoni kwa madai
kuwa kiongozi huyo anaendesha bunge hilo kibabe.
James Mbatia ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha NCCR
Mageuzi akizungumza na waandishi wa
habari leo Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Vyama vinne vyenye wa Wabunge kwenye
Bunge hilo, ambavyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Chama cha Wananchi (CUF) na chama cha Act Wazalendo.
Amesema wamefikia hatua ya kukubali kurejea bungeni
kutokana kukubali ombi la viongozi wa dini waliokutana nao kwenye kikao cha
siku mbili walichokaa jana na juzi ambapo katika kikao hicho Kilihudhiriwa
na viongozi mbali mbali wa dini ambapo kiliitishwa na viongozi hao kutaka suluhu
ya mtafaruku wa kisiasa unaendeleo nchini ili kulinusuru taifa na mchafuku
yanaweza kutokea.
Amesema nia ya vyama hivyo si kuleta fujo bali na kuijenga amani ya Tanzania, amedai
kuwa wamewaeleza Viongozi hao wa kidini sababu ya wao kutoka bungeni imetokana
na Naibu spika kutokuwa mzelendo kwa
hatua yake ya kutoweka maslahi ya taifa huku akiendelea kukitetea chama chake.
Hata hivyo,Mbatia amesema baada ya wabunge hao kukubali kurejea bungeni hatua inayofuta ni ya wao kututana na wabunge wote wa Upinzani na kuwaeleza
ombi lao hilo na kulitekeleza.
Kwa Upande wake Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
ACT-Wazalendo,Ado Shaibu amemtaka Rais John Magufuli kupeleka mswaada Bungeni
ambao ni wa kuvifuta vyama vya Upinzani ili abaki yeye awe anaongoza nchini.
Amesema hatua yake ya kuvikandamiza vyama vya
upinzani hakikubaliki huku akidai kuwa wao ACT-Wazalendo watapambana mpaka
kuhakikisha haki yao ya msingi inaheshimiwa ya kufanya siasa nchini.
Ameeleza kuwa kwa sasa wanangojea barua kutoka
Chadema ili nao waweze kujiiunga na Oparesheni ya Kupinga Udiktea nchini
(UKUTA).
KUHUSU MAANDAMANO
NA MIKITANO YA HADHARA TAREHE 1 SEPTEMBA.
Mbatia ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Vunju,amesema
kwa sasa wanaendelea na vikao usiku na mchana kuangalia kama kutapatikana
suluhu kwenye suala hilo.
Amesema kwa sasa viongozi wa dini waliokutana nao baada ya kuzungumza nao walipanga kukutana na Rais Magufuli huku wakiwahidi wakitoka huku
watakuja kuongea na Viongozi wa Upinzani.
Sanjari na hayo,Mbatia amelitadharisha jeshi la
Polisi nchini kuacha kutumika kisiasa kwa kuingiza mambo ya jeshi hilo na
siasa,
Amesema hatua ya jeshi hilo kuyahusisha mauaji ya
Polisi wa nne wa jeshi hilo lilotokea Mbagala Jijini hapa na kulisusisha na
harakati za siasa nchini ni kuliahabisha jeshi hilo na kuchangia kuleta hofu kwa
jamii.
Amedai kuwa hata katazo walilotoa kwa vyama vya
siasa kutofanya mikutano ya ndani kunazidi lionyesha jeshi hilo kufanya kazi
kichama zaidi.