Zinazobamba

WANAHABARI WAUCHOKA UTAWALA WA MAGUFULI MAPEMA,JUKWAA LA WAHARIRI NAO WAUJIA JUU,SOMA HAPO KUJUA



 Dk. John Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

SERIKALI ya Rais John Magufuli inalalamikiwa kutokana na serikali yake kujenga tabia ya ukandamizaji kwa wanahabari, anaandika Moses Mseti.

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza kusikitika kutokana na kujengekwa kwa tabia hiyo na kwamba, kitendo cha kunyang’anya uhuru na haki ya wananchi kupata habari hakikubaliki

Makamu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile amesema, kutokana na ukandamizaji unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli hauvumiliki.

Moja ya mambo na sheria zinazoonekana kuvikwaza vyombo vya habari nchini ni waandishi wa habari kuzuiwa kuchukua habari moja kwa moja ‘live’ wakati wa vikao vya bunge la bajeti na sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 pia kutungwa kwa sheria zinazokandamiza vyombo vya habari na waandishi wake.

Akizungumza leo wakati wa kilele cha Vyombo vya Habari Duniani (WPFD) amesema, kitendo cha serikali kuwazuia waandishi wa habari na vyombo vya habari kuonesha ‘live’ bunge hilo ni sawa na uvunjwanji wa Sheria na Haki ya Kupata Habari huku akidai kitendo hicho hawakubaliani nacho.

“Mwaka 1992 sheria za habari zilikuwa 17 lakini sasa hivi zimetengenezwa tengenezwa tu hadi kufikia 26 hiyo yote ni ya Serikali kutaka kuvibana vyombo vya habari visifanye kazi zao kwa uhuru, kitendo ambacho ni kibaya sana kwa ukuaji wa tasnia hii,” amesema Balile.
Pia Balile ametolea mfano sheria ya takwimu (The statistics act, 2013) ambayo anasema kuwa, sheria hiyo ipo kwa lengo la kumkandamiza mwanahabari na vyombo vya habari.
Na kwamba, kwenye kutekeleza wajibu wao na hawatarudi nyuma katika kutetea suala hilo mpaka pale litakapopatiwa ufumbuzi.
“Mfano kuna hili suala la takwimu ambalo linawanyima waandishi wa habari, kwamba kama mwandishi akiandika takwimu ambazo zitakuwa zimekosewa na mtoa taarifa, yeye ndie anaekuwa mhanga tatizo na wakati yeye kaandika,”alisema Balile.
Katika hatua nyingine Ubalozi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania umeeleza mambo 17 yanayolenga kulisaidia Taifa kupiga hatua ya maendeleo pamoja na vyombo vya habari nchini kukuwa kitaaluma kwa miaka 10.
Akiwasilisha malengo hayo 17 kwa wahariri, waandishi wa habari na wadau wa habari, Usiah Nkoma, Ofisa Habari UN amesema, malengo hayo yanakusudia kuleta maendeleo endelevu ya kiuchumi.
Nkoma ameyataja mambo hayo kuwa ni kutokomeza umaskini, kukomesha njaa, afya njema na ustawi, elimu bora, usawa wa jinsia, maji salama na safi, nishati mbadala kwa gharama ndogo, kazi zenye staha na ukuzaji uchumi.
Pia ametaja mambo mengine kuwa ni kukuzaviwanda na miundombinu, kupunguza tofauti za kiubinadamu, kuwa na miji na jamii endelevu, matumizi na uzalishaji wenye uwajibikaji, kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi, kuendeleza uhai katika maji.
Nkoma ametaja mambo mengine kuwa ni pamoja na kulinda uhai wa ardhi, amani, haki na taasisi madhubuti na ushirikiano katika kufanikisha malengo hayo endelevu kwa ukuaji wa uchumi wa taifa na vyombo vya habari kwa ujumla.
“Malengo yetu nikuona kila mmoja akiwajibika kwa nafasi yake na waandishi wa habari kwenye taifa lolote lile wao ndio nguzo kubwa kwa ukuaji wa maendeleo yaTaifa hilo ni lazima kuwepo na mazingira salama,” amesema Nkoma.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline

Hakuna maoni